Katibu Mkuu Wizara ya
Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel (wakwanza kushoto)
akiangalia mitambo ya kurushia matangazo ya Shirika la Utangazaji Tanzania(TBC)
wakati alipofanya ziara ya kikazi katika minara ya shirika hilo leo hii
Kisarawe. Profesa Elisante amefanya ziara katika Taasisi tatu zilizo chini ya
Wizara hiyo ambazo ni Baraza la Sanaa Tanzabia (BASATA),Tanzania Standard
Newspapers (TSN) na Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) lengo likiwa ni
kufahamiana na wafanyakazi,kuwahimiza kufanya kazi kwa bidii na kujua
changamoto zinazowakabili ikiwa ni kutimiza kauli mbiu ya Hapa Kazi Tu ya awamu
ya Tano. Anayefuatia ni Mkurugenzi Mkuu wa shirika hilo, Bw. Clement Mshana.
Katibu Mkuu Wizara ya
Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Prof Elisante Ole Gabriel akiangalia tofauti
ya santuri ya zamani na flashi ya kisasa zinavyozidiana ukubwa kwa
umbo alipotembelea maktaba mojawapo katika ofisi za shirika la utangazaji
Tanzania (TBC) alipofanya ziara kuongea na menejimenti ya shirika ilo leo
jijini Dar es Salaam.Santuri zilitumika kipinda shirika hilo likiitwa Radio
Tanzania Dar es Salaam.(RTD).
Katibu Mkuu Wizara ya
Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel (waliosimama watatu
kulia) akiwa katika mojawapo ya studio za kurushia matangazo ya shirika la
Utangazaji Tanzania (TBC) wwakati alipotembelea shirika ilo leo kuongea na
menejimenti yake pamoja na kuona utendaji wake.
Katibu Mkuu Wizara ya
Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel (aliyekaa mwenye
miwani) akipata maelekezo jinsi gazeti linavyotengenezwa kutoka kwa mtumishi wa
Standard News Papers (TSN) leo jijini Dar es Salaam alipofanya ziara ya kikazi
na kuangalia utendaji wa kazi.
Katibu Mkuu Wizara ya
Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Prof Elisante Ole Gabriel (wa pili kulia)
akiangalia moja ya kazi za vijana wanojifunza kutengeneza batiki na kuweka
chapa alipotembelea ofisi za Baraza la Sanaa Tanzania (Basata) leo hii jijini
Dar es Salaam. (Picha zote na Idara ya Habari-Maelezo)
No comments:
Post a Comment