Mkuu wa Kitengo cha Sheria na Mambo ya Uhusiano wa Kampuni ya Total Tanzania, Marsha Msuya-Kilewo, akizungumza na waandishi wa habari kuhusu shindano la ujasiriamali la Startupper of the Year 2016, kabla ya uzinduzi huo, jijini leo. Kulia ni Meneja Udhibiti wa kampuni hiyo, Olivier Cursente na kushoto ni Mwanzilishi na Ofisa Mtendaji wa Kampuni ya Problem Solved, Mhandisi na Mjasiriamali, Eric Mutta.
KAMPUNI ya Total ya Tanzania, yazindua Shindano la Total «Startupper of the year
by Total», lililobuniwa
na kundi la Makampuni ya Total litakaloshirikisha
nchi
34 za Afrika kwa wakati mmoja. Shindano hilo linalenga katika
kutambua, kuzawadia na kuwezesha
utekelezaji wa miradi bora ya biashara ya
ujasiliamali inayoanza au iliyobuniwa chini ya
miaka miwili kwa ajili ya maendeleo ya
jamii na taifa.
Washindi wa miradi bora watapewa tuzo ya « Startupper of the year 2016 by
Total » itakayoambatana
na fedha taslimu
itakayotumika kama mtaji wa kuendeleza,
na kusimamia uendeshaji
wa miradi hiyo.
Shidano hili ni bure kwa raia wote wa Watanzania wenye umri kati ya miaka kumi na nane( (18) hadi miaka thelathini na tano (35).
Fomu za maombi zimeanza kutolewa kuanzia tarehe 1 Novemba 2015 saa 2:00 asubuhi kwenye tovuti: http://startupper.total.com/. Shindano litakuwa wazi hadi Januari 31, 2016 saa 5:00 asubuhi ambapo ndio mwisho wa kurejesha fomu.
Jopo la Majaji linalohusisha wataalamu wa biashara, litachagua miradi kumi bora nchini Tanzania itakayoingia fainali kwa kuzingatia vigezo vya ubunifu, uhalisia na uwezo wa mradi katika kuleta maendeleo na kuboresha hali ya maisha ya jamii kubwa ya Watanzania.
Orodha ya washindi watakaoingia fainali itachapishwa tarehe 28, Februari, 2016 katika tovuti ile ile walipochukulia fomu za kugombea.
Kuanzia tarehe 15 Machi, 2016, Washindi hao kumi, wataingia katika mchuano wa fainali kutafuta tatu bora ambapo washindi watawajibika kuitetea miradi yao mbele ya jopo la majaji ili kupata miradi mitatu bora ambapo mshindi wa jumla atatangazwa na kupewa zawadi katika hafla maalum ya utoaji wa tuzo.
Sheria,
taratibu,
kanuni na vigezo vya shindano
hili
zinapatikana bure kwenye tovuti ya (http://startupper.total.com/).
Shindano la « Startupper of the year by Total » ni juhudi za Kampuni ya kimataifa ya Total katika kuhamasisha maendeleo ya kiuchumi na kijamii ili kusaidia nchi zote duniani ambako kampuni ya Total ipo.
Shindano la « Startupper of the year by Total » ni juhudi za Kampuni ya kimataifa ya Total katika kuhamasisha maendeleo ya kiuchumi na kijamii ili kusaidia nchi zote duniani ambako kampuni ya Total ipo.
Shindano hili ni hatua madhubuti yenye
lengo la kuvumbua ubunifu wa miradi mbalimbali ya
maendeleo yenye lengo la kuchangia uanzishwaji
wa viwanda vidogo vitakavyotoa ajira na kuchangia maendeleo ya
jamii na ya nchi za bara la Afrika kwa
ujumla. Shindano hili linalenga
kuibua miradi mipya, iliyotokana na
wananchi wenyewe ambayo inaendana na malengo ya jumla
ya uwepo wa kampuni ya Total.
No comments:
Post a Comment