TANGAZO


Thursday, November 5, 2015

Jeff aachia video ya wimbo wake mpya wa 'Mama Afrika" unaotangaza utalii wa Tanzania

jeff

Mwanamuziki aliyewahi ishi nchini Tanzania na pia mwenye asili ya Congo, Jeff Maximum ambaye anaishi Ughaibuni katika shughuli zake za Muziki katika pozi ambapo kwa sasa ameachia video ya wimbo wake mpya wa "Mama Afrika" ambao wimbo huo unatangaza Utalii wa Tanzania.

Na Mwandishi Wetu
MWANAMUZIKI anayefanya kazi zake nchini Marekani na Dubai, Jeff Maximum tayari ameshaachia video ya wimbo wake mpya uitwao “Mama Afrika” ambao umetayarishwa Bagamoyo Nchini Tanzania hivi karibuni.

Kwa mujibu wa Jeff anaweka wazi kuwa, kuwa video hiyo iliyoachiwa Novemba 2 mwaka huu, tayari imeshaanza kuonekana katika vituo mbalimbali vya televisheni Bara la Afrika ikiwemo nchini, pia katika nchi za Nigeria, Afrika Kusini, Kongo, Ghana, Kenya na kwingineko.

Pia video hiyo inaonekana katika vituo vya televisheni vya nchini Uingereza, Dubai, Amerika na kwingineko huku ikitangaza utalii wa Tanzania kwa asilimia kubwa.
Jeff anaweka wazi kuwa, aliamua kuitayarishia video hiyo nchini Tanzania kwa kuwa ni kati ya nchi nyingi anazozipenda zaidi Barani Afrika.

Na kuongeza kuwa, video hiyo imetengenezwa na mwongozaji anayechipukia kutoka Tanzania Hanscana (Wanene Films), huku audio yake ikiwa imetayarishwa katika studio yake iliyopo nchini Dubai (One Vision Records).
Tazama video hiyo hapa chini.

No comments:

Post a Comment