Waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu ataubadilisha uteuzi wa mkurugenzi mpya wa mawasiliano kufuatia tamko alilotoa akimkosoa rais Barrack Obama wa Marekani na watu wengine,Marekani imesema.
Katika mtandao wa facebook Ran Baratz amemshtumu Obama akisema ana chuki dhidi ya wayahudi na kumtaja waziri wa maswala ya kigeni nchini Marekani John Kerry kama aliye na fikra za mtoto mdogo asiyezidi umri wa miaka 12.
Bwana Netanyahu ameelezea matamshi hayo kama yasiokubalika.
Anatarajiwa ikuku ya White House wiki ijayo kwa mkutano kati ya Israel na Marekani.
Maafisa wa Israel wanasema kuwa bwana Baratz hataandamana naye.
Msemaji wa idara ya maswala ya ndani nchini Marekani John Kirby amesema chapisho la bwana Baratz katika mtandao wa facebook 'linasumbua na kukera'.
Amesema:Tunataraji kwamba maafisa wa serikali kutoka taifa lolote hususan washirika wetu watazungumza kwa heshima na ukweli kuhusu maafisa wakuu wa serikali ya Marekani.
Waziri mkuu Netanyahu alizungumza na waziri wa maswala ya Kigeni bwana John Kerry na tunaelewa kwamba uteuzi huo utabadilishwa wakati atakaporudi kutoka ziara yake ya Marekani.
Chapisho hilo lilionekana muda mfupi baada ya Netanyahu kutangaza uteuzi wa Bwana Baratz kama msemaji wake mkuu siku ya jumatano.
No comments:
Post a Comment