TANGAZO


Monday, November 16, 2015

Hungary waingia fainali Euro 2016

Image captionTimu ya taifa ya Hungary
Timu ya taifa ya Hungary imefuzu kutinga hatua ya fainali za Mataifa ya Ulaya, Euro 2016, baada ya kuifunga Norway 2-1 katika mchezo wa mchujo.
Hii ni mara ya kwanza kwao kufika fainali za mashindano makubwa tangu mwaka 1986.
Mchezaji Tamas Priskin ndiye aliyeanza kuwafungia Hungary bao la kwanza dakika ya 13 kisha Örjan Nyland, wa Norway akajifunga. Markus Henriksen, aliifungia timu yake ya Norway bao pekee.
Ushindi huo umewafanya wafuzu kwa jumla ya Mabao 3-1 katika michezo mechi mbili baada ya kushinda mechi ya kwanza Ugenini kwa bao 1-0.
Zimesalia timu tatu zinazowania kufuzu kwa fainali za Euro 2016.
Leo kutachezwa mchezo mwingine mmoja wa kusaka tiketi ambapo Ireland watakipiga na Bosnia na Herzegovina.

No comments:

Post a Comment