TANGAZO


Tuesday, November 10, 2015

Dk. Kimei aongoza harambe ya ujenzi wa Kanisa la KKKT Usharika wa Siha mkoani Kilimanjaro

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei akizungumza wakati wa ibada maalum iliyofanyika katika Kanisa la KKKT Usharika wa Siha Sango Mkoani Kilimanjaro. Ibada hiyo ilikwenda sambamba na harambee ya kuchangia ujenzi wa kanisa hilo ambapo zaidi ya shs Milioni 100 zilipatikana. (Picha zote na Francis Dande)
Mchungaji Kiongozi wa Kanisa la Kiijili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Cuthbert Temba akiongoza ibada.
Waumini wa Kanisa hilo wakiwa katika ibada.
Katibu Mkuu wa Dayosisi ya Mashariki na Pwani, Goodfrey Nkini na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei wakiwa kanisani na Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa CRDB, Huduma Shirikishi, Esther Kitoka.
Mkurugenzi Benki ya CRDB tawi la Moshi, Francis Mollel (kulia) akipokea mbuzi kutoka kwa Mchungaji Kiongozi wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Usharika wa Siha Sango, Cuthbert Temba (wa pili kushoto) katika harambee ya  kuchangia ujenzi wa Kanisa la KKKT Usharika wa Siha Sango. Wa pili kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei  akimkabidhi mbuzi Mchungaji Emmanuel Kileo baada ya wakati wa harambee ya kuchangia ujenzi wa Kanisa hilo. Kushoto ni Solomon Nkini.
Katibu Mkuu wa Dayosisi ya Mashariki na Pwani, Goodfrey Nkini akipokea mbuzi baada ya kumnunua katika harambee ya ujenzi wa Kanisa la KKKT Usharika wa Siha.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei akimkabidhi ng’ombe Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa  Beki  ya CRDB, Huduma Shirikishi, Esther Kitoka (kushoto) katika harambee ya kuchangia ujenzi wa Kanisa.
Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Huduma Shirikishi, Esther Kitoka, akipokea kuku kutoka kwa Katibu wa Idara ya Udiako wa Dayosisi ya Kaskazini, Julius Lema.
Mkurugenzi wa Masoko, Utafiti na Huduma kwa Wateja wa Benki ya CRDB, Tully Mwambapa akiwa amepozi kwa picha na mzee Godfriend Kileo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei akipokea kuku kutoka kwa Mchungaji Kiongozi wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Usharika wa Siha Sango, Cuthbert Temba.
Meneja Uhusiano wa Benki ya CRDB, Godwin Semunyu akikabidhi mchango wa shs. milioni 5 kwa mgeni rasmi Dk. Kimei.
Mkurugenzi wa Masoko, Utafiti na Huduma kwa Wateja wa Benki ya CRDB, Tully Mwambapa akikabidhi mchango wa shs milioni 5 kwa mgeni rasmi Dk. Kimei.
Dk. Charle Kimei akikabidhi mchango wa shs. milioni 18 kwa Mchungaji Kiongozi wa Kanisa la KKKT Usharika wa Siha Sango.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei akimpongeza mzee Godfriend Kileo baada ya kuchangia kiasi cha Shs. Milioni 4.5 katika harambee hiyo.
Mkurugenzi wa Masoko, Utafiti na Huduma kwa Wateja wa Benki ya CRDB, Tully Mwambapa akizungumza wakati wa hafla hiyo.
  Mkurugenzi wa Masoko, Utafiti na Huduma kwa Wateja wa Benki ya CRDB, Tully Mwambapa akimkabidhi Mbuzi mzee Godfriend Kileo wakati wa harambee hiyo.
 Ibada ikiendelea.
 Waumini wakiwa katika ibada.
Bendi ya GMK ikiimba nyimbo za injili.
Waumini wa Kanisa la KKKT Usharika wa Siha Sango wakiwa nje ya kanisa hilo.

No comments:

Post a Comment