TANGAZO


Wednesday, November 18, 2015

Changamoto za Pamba nchini kupatiwa ufumbuzi

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Chakula na Ushirika Bwana  Zidikheri Mundeme akihutubia wadau wa pamba hivi karibuni katika ukumbi wa Hoteli ya White Sand jijini Dar es salaam. (Picha zote na mpigapicha wetu)
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Chakula na Ushirika Bwana  Zidikheri Mundeme akisalimiana na wadu wa pamba baada ya kumaliza hotuba yake ilyohusu  mikakati ya kuimarisha kilimo cha pamba hapa nchini. 
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Chakula na Ushirika Bwana  Zidikheri Mundeme akisalimiana na wadu wa pamba baada ya kumaliza hotuba yake ilyohusu mikakati ya kuimarisha kilimo cha pamba hapa nchini. 

Na Mwandishi wetu
NIBU Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Chakula na Ushirika Bwana  Zidikheri Mundeme amewataka wadau  wa zao la pamba kuwalinda wakulima wadogo wa zao hilo kwa kuwapatia  mbegu bora na madawa sahihi ili kuboresha zao hilo.

Akiongea  wakati wa ufunguzi wa mkutano wa wadau wa zao hilo kutoka Kenya, Brazili na vituo mbalimbali vya utafiti vya hapa nchini uliofanyika katika ukumbi wa hoteli ya White sand hivi karibuni,Bwana   Mundeme amesema kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa  nguvu za ziada zinahitajika katika kumsaidia mkulima mdogo wa pamba hapa Tanzania.

"Kilimo cha mkataba,ukosefu wa soko na uongezaji wa thamani na kipato kidogo cha wakulima wa zao hilo ni baadhi ya changamoto zinazomkabili mkulima mdogo wa pamba   ambapo  mkutano huu unatakiwa kuzitafutia utatuzi changamoto hizo" aliongeza Bwana   Mundeme.


Aidha amevipongeza vituo vya utafiti vya Kanda ya Ziwa kikiwemo kituo cha utafiti Ukiriguru ambacho kilitafiti mbegu mpya ya pamba  aina ya UKM 08 ambayo imekuwa ikifanya vizuri sana kwa wakulima.

No comments:

Post a Comment