Bunge la Myanmar limefunguliwa kwa kikao chake cha mwisho kabla ya maamuzi ya matokeo ya uchaguzi wa wiki jana kuanza kutekelezwa.
Katika uchaguzi huo,chama cha upinzani (National League for Democracy)NLD cha bi Aung San Suu Kyi, kilishinda viti vingi zaidi.
Japo chama hicho cha NLD kilishinda kwa asilimia 80 chama kilichopo sasa madarakani kinachoungwa mkono na jeshi la nchi hiyo cha Union Solidarity and Development Party kitaendelea kuwa na ushawishi mkubwa hadi hapo kitakapokabidhi madaraka hapo Januari.
Msemaji wa chama NLD Nyan Win amesema chama hicho kitashirikiana na upinzani kuhakikisha amani na uwiano nchini humo haswa wakati huu wa mpwito.
Bi Aung San Suu Kyi hakusema chochote alipowasili bungeni.
No comments:
Post a Comment