Siku moja baada ya rais wa Nigeria Muhammadu Buhari kumfuta kazi mkuu wa taasisi ya kupambana na rushwa nchini humo Economic and Financial Crimes Commission (EFCC).
Kamishna wa polisi bwana Ibrahim Mustafa Magu ndiye ameteuliwa kuiongoza EFCC kama kaimu mkuu.
Msemaji wa rais Buhari, Garba Shehu, amesema kuwa kamishna wa polisi bwana Mustafa Magu atachukua usukani katika taasisi hiyo ya kupambana dhidi ya rushwa.
Hakuna sababu zilizotolewa kwa kumpiga kalamu Ibrahim Lamorde,ambaye ameshikilia wadhifa huo tangu 2011.
Hata hivyo Mwezi Agosti, Lamorde alikanusha madai kuwa takriban dola bilioni 5 zilikuwa zimetoweka katika akaunti za benki za tume hiyo.
Wakati huo bwana Lamorde alisema wanaoeneza uvumi huo walikuwa wanamtupia tope tu kwani haikuwa ukweli.
Mwaandishi wa BBC nchini Nigeria anasema Rais Buhari anataka kuhakikisha kwamba mawaziri wapya atakao wateua hawatatumia ofisi kujinufaisha.
Baraza lake la mawaziri linatarajiwa kuapishwa baadaye wiki hii, zaidi ya miezi tano baada ya kuingia madarakani.
Rais Buhari alishinda kiti cha urais mwezi Machi, katika uchaguzi mkuu wa kihistoria na akaahidi kupambana na rushwa na ubadhirifu wa mali ya umma.
Rais Buhari anadhaniwa kuwa na mitazamo ya kiimla ikija kwa maswala ya kupambana na ufisadi uliokithiri nchii humo na hivyo inadaiwa kuwa amechelewa kuapisha baraza lake la mawaziri kwa zaidi ya miezi 5 ilikupiga msasa kikamilifu mawaziri wake.
Rais huyo anaamini kuwa ubadhirifu wa mali ya umma na ufisadi ndio unaoizuia nigeria kunawiri ipasavyo licha ya kuwa na uchumi mkubwa zaidi barani Afrika.
No comments:
Post a Comment