Kijana raia wa Uingereza ambaye aliingia katika njia ya magari yakiwa kasi Mahakama ya Singapore imemtupa jela wiki sita jela.
Kijana Yogvitam Pravin Dhokia, mwenye miaka 27, aliingilia njia ya mbio za magari ili achukue picha. Alifanya tendo hilo mwezi septemba wakati wa Singapore Grand Prix.
Kijana huyo alikubali kosa hilo alilolifanya katikati ya njia ya magari ya Fomula 1 ambayo yalikuwa yanakimbia kwa kasi ya 280km/h (175mph).
Akitangaza hukumu hiyo, Jaji Chay Yuen Fatt alisema, kuingilia kokote njia ya magari kunaweza na kungeweza kusababisha ajali mbaya.
Mwanasheria aliyekuwa anamtetea kijana huyo aliiambia mahakama kuwamteja wake hakuwa na leo la kuingilia mashindano lakini anakubali kubwa tendo lake lilikuwa la kitoto.
No comments:
Post a Comment