Mwanasheria kutoka Chama Cha Wanasheria Wanawake Tanzania (TAWLA) Edna Kamaleki, akiwasilisha mada mbalimbali wakati wa mdahalo wa kujadili amani wakati wa uchaguzi unaotarajiwa kufanyika Oktoba 25 mwaka huu.
Mmoja wa washiriki wa mdahalo huo wa TAWLA, akielezea jambo.
Mwanasheria kutoka TAWLA, Edna Kamaleki, akielezea jambo wakati akiwasilisha mada mbalimbali kwenye mdahalo huo juzi.
Baadhi ya Watendaji wa Tawla wakiandika baadhi ya maoni ya washiriki wa mdahalo huo.
Mjumbe wa Serikali ya Mtaa Pugu jijini Dar es Salaam Jamila Jackson, akichangia hoja ya mjadala huo. Ofisa Ustawi wa Jamii Manispaa ya Ilala, Victor Mukiza, akichangia mada ya amani wakati wa mdahalo ulioandaliwa na chama cha Wanasheria Wanawake Tanzania (TAWLA) kwa watendaji wa Serikali za Mitaa,Polisi na watumishi wa Halmashauri hiyo juzi.
Mwanasheria wa Manispaa ya Ilala, Elizabeth Buwimba, akichangia mada ya wajibu wa mwanamke kushiriki kwenye uchaguzi na umuhimu wa kufanya hivyo wakati wa mdahalo wa kujadili amani wakati na baada ya uchaguzi, uliofanyika eneo la Pugu jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya washiriki wakimsikiliza Mwanasheria kutoka Chama Cha Wanasheria Wanawake (TAWLA) Edna Kamaleki wakati wa mjadala wa amani wakati wa uchaguzi mkuu, eneo la Pugu jijini Dar es Salaam juzi. Mdahalo uliohusisha Jeshi la Polisi watendaji wa mitaa wananchi na watendaji wa Halmashauri.
No comments:
Post a Comment