Pages

Saturday, October 17, 2015

Rais Kikwete, Magufuli wauaga mwili wa marehemu Filikunjombe jijini Dar es Salaam

Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete na mgombea Urais wa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dkt. John Pimbe Magufuli wakitoa heshima za mwisho mbele ya majeneza ya aliyekuwa Mbunge wa Ludewa(CCM) Marehemu Deo Filikunjombe na wenzake wawili waliofariki katika ajali ya helikopta juzi katika pori la akiba la mbuga ya Selous. Marehemu aliagwa katika Hospitali ya jeshi Lugalo jijini Dar es Salaam leo. 
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akimfariji Mke wa Marehemu Bi Sarah Filikunjombe wakati wa kuaga mwili wa marehemu katika hospitali ya jeshi Lugalo jijini Dar es Salaam leo. (Picha zote na Freddy Maro)

No comments:

Post a Comment