Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, Waziri wa Fedha Bibi Saada Mkuya na Gavana wa Benki Kuu Professa Benno Ndulu wakiwa katika picha ya pamoja na Maofisa waandamizi wa benki kuu pamoja na wafanyakazi wa Benki kuu Tawi jipya la Dodoma muda mfupi baada ya hafla wa uzinduzi wa tawi hilo.
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akisaini kitabu cha wageni mashuhuri wakati wa hafla ya ufunguzi wa jengo la Tawi jipya la Benki Kuu mjini Dodoma leo huku Waziri wa Fedha Bibi Saada Mkuya na Gavana wa Benki Kuu Profesa Benno Ndulu wakishuhudia.
Rais Kikwete na Waziri wa Fedha Saada Mkuya wakipiga makofi baada ya kufunua pazia la uzinduzi huo.
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, Waziri wa Fedha bibi Saada Mkuya, Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za serikali Professa Musa Assad na Katibu Mkuu Hazina Dkt. Servacious Likwelile wakikata utepe kufungua jengo la ofisi za CAG mjini Dodoma jana.
Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali Professa Musa Assad akimkabidhi Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete kitabu kinachohusu kanuni na utendaji wa kazi za ofisi yak e wakati wa uzinduzi wa jengo la Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali uliofanyika mjini Dodoma jana.
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, Waziri wa Fedha Bibi Saada Mkuya(Wanne kushoto),Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali Professa Mussa Assad(wapili kushoto), Katibu Mkuu Hazina Dkt.Servacius Likwelile (kulia) na Mkuu wa Mkoa wa Dodoma wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali iliyofunguliwa rasmi mjini Dodoma jana.
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akifunua kitambaa kufungua rasmi jengo la Wizara ya Fedha mjini Dodoma jana. Kulia ni Waziri wa Fedha Bibi Saada Mkuya.
Baadhi ya Watumishi kutoka Benki Kuu,Hazina na Ofisi ya Mdhibiti na mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali wakisikiliza hotuba ya Rais Kikwete muda mfupi baada ya kufungua majengo matatu ya taasisi hizo mjini Dodoma jana.
Baadhi ya Watumishi kutoka Benki Kuu,Hazina na Ofisi ya Mdhibiti na mkaguzi Mkuu wa Hesabu za serikali wakisikiliza hotuba ya Rais Kikwete muda mfupi baada ya kufungua majengo matatu ya taasisi hizo mjini Dodoma jana.
Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza na watumkshi wa Wizara ya Fedha,Benki Kuu pamoja na wale kutoka ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za serikali muda mfupi baada ya kuzindua majengo matatu ya taasisi hizo mjini Dodoma jana. (Picha zote na Freddy Maro)

No comments:
Post a Comment