TANGAZO


Sunday, September 6, 2015

Mgombea wa Ukawa, Edward Lowassa apasua anga Mjini Nzega Tabora

Waziri Mkuu Mstaafu,Mh.Fredrick Sumaye akihutubia Mkutano wa hadhara wa Kampeni za Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika mwamvuli wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, uliofanyika kwenye Uwanja wa Polisi Nzega, leo Septemba 6, 2015.Kushoto ni Mwenyekiti wa CHADEMA, Mh. Freeman Mbowe. (Picha zote na Othman Michuzi)
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika mwamvuli wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, akiambatana na Mwenyekiti wake, Mh. Freeman Mbowe wakiwasili kwenye Uwanja wa Polisi Nzega, leo Septemba 6, 2015, kulikofanyika Mkutano wa Kampeni zake. 
Baadhi ya wananchi wa Mji wa Nzega, Mkoani Tabora wakimshangilia Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika mwamvuli wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, wakati wa Mkutano wa hadhara wa Kampeni, uliofanyika kwenye Uwanja wa Polisi Nzega, leo Septemba 6, 2015. 
Baadhi ya wananchi wa Mji wa Nzega, Mkoani Tabora wakimshangilia Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika mwamvuli wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa,wakati wa Mkutano wa hadhara wa Kampeni, uliofanyika kwenye Uwanja wa Polisi Nzega, leo Septemba 6, 2015. 
Mgombea wa Ukawa aliyeteuliwa kuwania Ubunge wa Jimbo la Nzega Mjini kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), akizungumza na wananchi wake kabla ya kupigiwa kura ya wazi iliyompitisha kuwania nafasi hiyo na kumtupa nje Mwezake wa Chama cha CUF, Mezza Leonard (hayupo pichani), wakati wa Mkutano wa hadhara wa Kampeni za Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika mwamvuli wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassauliofanyika kwenye Uwanja wa Polisi Nzega, leo Septemba 6, 2015.Kushoto ni Mwenyekiti wa CHADEMA, Mh. Freeman Mbowe. 
Mmoja wa wananchi wa wananchi wa Mji wa Nzega, Mkoani Tabora akiwa juu ya baiskeli ili aweze kumuona na kumsikiliza vyema Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika mwamvuli wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, alipokuwa akitangaza sera zake katika Mkutano wa Kampeni, uliofanyika kwenye Uwanja wa Polisi Nzega, leo Septemba 6, 2015. Kushoto ni Mwenyekiti wa CHADEMA, Mh. Freeman Mbowe.

No comments:

Post a Comment