TANGAZO


Monday, August 10, 2015

Wahubiri wa TZ waliotekwa kuwachiliwa

Watu wanaosali katika msikiti
Mtu anayeongoza mazungumzo ya kuachiliwa huru kwa wahubiri saba wa kiislamu kutoka Tanzania waliotekwa nyara wiki iliopita ameiambia BBC kwamba makubaliano ya kuwaachilia huru huenda yakaafikiwa hivi karibuni.
Sheikh Suleiman Mohammed amesema kuwa kundi la watu wanaofanya mazungumzo hayo limewasiliana na watekaji nyara hao na kwamba viongozi hao wa dini hawajateswa.
''Wametaka kupewa fedha ili kuwahudumia mateka hao iwapo fedha za fidia hazitalipwa'',aliambia BBCswahili.
Ameongezea kuwa maimamu hao sio waliokuwa wakilengwa na washambuliaji hao na kwamba walikuwa katika mahala pabaya katika wakati usiofaa.

No comments:

Post a Comment