TANGAZO


Tuesday, August 11, 2015

Ugiriki yakubaliana na wakopaji wake



waziri wa fedha nchini Ugiriki Tsokalotos
Ugiriki inasema kuwa imekubaliana na wakopaji wake mpango wa kuikwamua kutoka kwa deni lake kulingana na waziri wa fedha nchini humo Euclid Tsakalotos.
Hatahivyo kuna maswala mawili ama matatu ambayo bado hatujayaangaiza na wakopaji hao alisema Tsakalotos.
Makubaliano hayo yalihitajika ili kulifanya taifa hilo lisalie katika muungano wa Ulaya na kukwepa kufilisika.
Serikali ya Ugiriki ina matumaini ya kulishawishi bunge la taifa hilo kupitisha makubaliano hayo ya kulipa deni hilo la yuro bilioni 86 kwa mpango wa miaka mitatu baadaye wiki hii.
Taifa hilo linahitaji makubaliano kuafikiwa ifikiapo Agosti 20,wakati ambapo taifa hilo linatarajiwa kulipa deni la yuro bilioni 3 kwa benki kuu ya Ulaya.

No comments:

Post a Comment