TANGAZO


Saturday, August 8, 2015

Serikali kuendelea kutekeleza miradi itakayowezesha kuwainua vijana kiuchumi

Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bi. Sihaba Nkinga akiongea na Maofisa Vijana na kuwataka kutumia elimu na ujuzi walioupata katika mafunzo ya ujasiriamali na ubunifu katika kuisaidia serikali kutimiza dhamira yake ya kuwainua vijana kiuchumi, wakati wa hafla ya ufungaji wa mafunzo ya ujasiriamali na ubunifu kwa Maafisa Vijana jijini Arusha. 
Mkurugenzi Mkuu wa Chuo cha Uongozi cha Mashariki na Kusini mwa Afrika (ESAMI) Prof Bonard Mwape akiwaeleza maafisa vijana kuhusu umuhimu wa kubadilisha fikra za vijana ili kuwawezesha kujiajiri kupitia mafunzo watakayowapatia ya ujasiriamali, wakati wa hafla ya ufungaji wa mafunzo ya ujasiriamali na ubunifu kwa Maafisa Vijana jijini Arusha. 
Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bi. Sihaba Nkinga akimkabidhi mmoja wa baadhi ya Maofisa Vijana vyeti vya kuhitimu mafunzo ya Ujasiriamali na ubunifu, wakati wa hafla ya ufungaji wa mafunzo ya ujasiriamali na ubunifu kwa Maafisa Vijana jijini Arusha. 
Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bi. Sihaba Nkinga akimkabidhi mmoja wa baadhi ya Maofisa Vijana vyeti vya kuhitimu mafunzo ya Ujasiriamali na ubunifu, wakati wa hafla ya ufungaji wa mafunzo ya ujasiriamali na ubunifu kwa Maafisa Vijana jijini Arusha.  
Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bi. Sihaba Nkinga akimkabidhi mmoja wa baadhi ya Maofisa Vijana vyeti vya kuhitimu mafunzo ya Ujasiriamali na ubunifu, wakati wa hafla ya ufungaji wa mafunzo ya ujasiriamali na ubunifu kwa Maafisa Vijana jijini Arusha.  
Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bi. Sihaba Nkinga akimueleza jambo Mkurugenzi Mkuu wa Chuo cha Uongozi cha Mashariki na Kusini mwa Afrika (ESAMI) Prof.Bonard Mwape wakati wa hafla ya ufungaji wa mafunzo ya ujasiriamali na ubunifu kwa Maafisa Vijana jijini Arusha. 
Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bi. Sihaba Nkinga na Mkurugenzi Mkuu wa Chuo cha Uongozi cha Mashariki na Kusini mwa Afrika (ESAMI) Prof. Bonard Mwape wakiwa katika picha ya pamoja na Maafisa Vijana na Baadhi ya watumishi wa Wizara ya Habari na Chuo cha ESAMI.

(Picha zote na Hassan Silayo-Maelezo)

Na Hassan Silayo-Maelezo, Arusha
SERIKALI ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania itaendelea kuweka mipango endelevu ya kuwasaidia vijana ili waweze kujiajiri na kuajiri wengine.

Hayo yamesemwa leo Jijini Arusha na Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bi. Sihaba Nkinga wakati akifunga mafunzo ya ujasiriamali na ubunifu yaliyotolewa kwa Maafisa Vijana.

Sihaba alisema kuwa kundi la vijana ni kundi kubwa lenye changamoto nyingi za kiuchumi na kijamii zinazopelekea kupunguza ufanisi katika uzalishaji mali kuanzia ngazi ya familia na taifa kwa ujumla

“Serikali inadhamira ya dhati ya kuwawezesha vijana kiuchumi kupitia miradi mbalimbali ya kimaendeleo ili kuwafanya vijana waweze kujikimu kimaisha kwa kujiajiri au kuajiri wengine na hii inatokana na serikali kutambua changamoto zinazowakabili vijana ikiwa ni kundi muhimu katika jamii” Alisema Sihaba.

Aidha Sihaba aliwataka Maafisa Vijana kutumia elimu na ujuzi walioupata katika mafunzo hayo katika kuisaidia serikali kutimiza dhamira yake ya kuwainua vijana kiuchumi na kulifanya kundi hilo kushiriki kikamilifu katika shughuli za uzalishaji mali kwa manufaa yao na Taifa kwa ujumla.

Naye Mkurugenzi Mkuu wa Chuo cha Uongozi cha Mashariki na Kusini mwa Afrika (ESAMI) Prof Bonard Mwape aliishukuru Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo kwa kuwapa nafasi ya kutoa mafunzo hayo kwa Maafisa Vijana watakayo yatumia katika kuwabadilisha fikra vijana na kuwafanya waweze kujiajiri kupitia ujasiriamali.

Prof. Mwape aliongeza kuwa huu ni mwanzo wa mambo mazuri yanayokuja kwa ajili ya vijana na kwa ushirikiano na Serikali kupitia Wizara watahakikisha vijana wanakuwa wanakuwa sehemu muhimu katika jamii hasa katika shughuli za uzalishaji mali.

Akizungumzia kuhusu faida za mafunzo hayo Afisa Maendeleo ya Jamii wa Jiji la Arusha Bi. Hanifa Ramadhani alisema kuwa watatumia mbinu walizojifunza katika mafunzo hayo ili kukidhi mahitaji ya vijana na kuwawezesha kujiajiri kupitia ujasiriamali na kuwafanya kushiriki katika shughuli za uzalishaji mali.

Mafunzo hayo ya Ujasiriamali na Ubunifu yameandaliwa kwa ushirikiano wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo na Chuo cha Uongozi cha Mashariki na Kusini mwa Afrika (ESAMI) kwa lengo la kuwawezesha vijana kujiajiri na kuajiri wengine.

No comments:

Post a Comment