Rais wa Jamhuri ya
Muungano ya Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete akibonyeza kitufe kuashiria
kuzinduliwa kwa Benki ya Maendeleo ya Kilomo nchini ambayo wakulima watapata
huduma za kibenki ikowemo mikopo na kuwainua wakulima waweze kulima kwa uwezo
wao. Hafla ya uzinduzi ilifanyika wakati wa kufunga Sherehe za Nane Nane
Kitaifa mwaka huu zilizofanyika mwishoni mwa wiki katika uwanja wa Ngongo
mkoani Lindi.
Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, mhe. Stephen
Wasira akimaribisha Mgeni Rasmi, Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Dkt.
Jakaya Kikwete kuongea na wakulima na wafugaji wakati wa kufunga Sherehe za
Nane Nane Kitaifa zilizofanyika mwishoni mwa wiki katika uwanja wa
Ngongo mkoani Lindi.
Mwenyekiti wa Chama
cha Kilimo Taifa (TASO) Englebert Moyo akitoa taarifa ya chama hicho kwa Mgeni
Rasmi, Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete kuongea na
wakulima na wafugaji wakati wa kufunga Sherehe za Nane Nane Kitaifa mwaka huu
zilizofanyika mwishoni mwa wiki katika uwanja wa Ngongo mkoani Lindi.
Mkuu wa Mkoa wa Lindi
Mwantumu Mahiza akitoa salamu za mkoa wa Lindi kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano
ya Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete wakati wa kufunga Sherehe za Nane Nane Kitaifa
zilizofanyika mwishoni mwa wiki katika uwanja wa Ngongo mkoani Lindi. Baadhi ya wananchi wakisikiliza hotuba ya kufunga Sherehe za Nane Nane Kitaifa zilizofanyika mwishoni mwa wiki katika uwanja wa Ngongo mkoani Lindi kwa kuongozwa na kauli mbiu: “Matokeo Mkubwa Sasa, Tuchague Viongozi Bora kwa Maendeleo ya Kilimo na Ufugaji”.
Baadhi ya wananchi wakisikiliza hotuba ya kufunga Sherehe za Nane Nane Kitaifa zilizofanyika mwishoni mwa wiki katika uwanja wa Ngongo mkoani Lindi kwa kuongozwa na kauli mbiu: “Matokeo Mkubwa Sasa, Tuchague Viongozi Bora kwa Maendeleo ya Kilimo na Ufugaji”.
Baadhi ya wananchi
wakitembelea baadhi ya bustani wakati wa kufunga Sherehe za Nane Nane Kitaifa
zilizofanyika mwishoni mwa wiki katika uwanja wa Ngongo mkoani Lindi. (Picha zote
na MAELEZO, Lindi Eleuteri Mangi-)
Na Eleuteri Mangi-Lindi
WATANZANIA wameaswa
kuboresha sekta ya kilimo ili kuleta mapinduzi ya kijani katika sekta hiyo kwa
kuzingatia na kutekeleza sera ya kilimo kwa manufaa ya wananchi wote na taifa
kwa ujumla.
Kauli hiyo imetolewa na
Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania Dkt. Jakaya Kikwete mwishoni mwa wiki
alipokuwa akiwaaga wakulima na wafuagaji wakati wa kufunga Sherehe za Nane Nane
Kitaifa zilizofanyika mwishoni mwa wiki katika uwanja wa Ngongo mkoani Lindi.
Rais Kikwete alisema
kuwa amewaaga Watanzania ambapo anamini sekta ya kilimo, uvuvi na ufugaji wa wanyama pamoja na ufugaji wa
nyuki nchini zimeongeza kutoa ajira na pato la taifa ambapo kilimo pekee kinachangia asilimia 25 hali
inayowahakikishia wananchi kuwepo kwa chakula cha kutosha pamoja na malighafi.
Changamoto hizo
zinazorudisha nyuma kilimo ni pamoja na matumizi ya jembe la mkono, kutegemea
mvua ya Mwenyezi Mungu ambayo nayo inakabiliwa na mabadiliko ya tabia nchi na
matumizi ya mbegu za asili ambazo hazizai sana kulinganisha na mbegu za kisasa.
Changamoto nyingine ni
matumizi madogo ya mbolea ambapo ardhi haina virutubisho vyote vinavyotakiwa
ili kupata mazao ya kutosheleza mahitaji kulingana na idadi ya watu na kuwa na chakula
cha ziada.
Ujuzi mdogo wa wakulima
katika kupanda mbegu mashambani nao umekuwa kikwazo katika mapinduzi ya kilimo
ambapo Rais alitoa mfano ambao unaonesha kuwa zao la mhogo likipandwa kitaalam
heka moja inapaswa kuwa na miche 2500 ili kutoa mazao bora na yenye tija ukilinganisha
na hali ilivyo sasa nchini.
Sasa Tanzania na Afrika
imeanza safari ya kulipeleka jembe la mkono kwenye jumba la makumbusho” alisema
Rais Kikwete.
Akionesha mafanikio
katika kilimo katika uongozi wake Rais Kikwete alisema kuwa utegemezi wa jembe
la mkono umepungua kutoka asilimia 62 hadi 70, matumizi ya wanyama kazi kwa
ajili ya kilimo yameongezeka kutoka asilimia 20 hadi 24 na matrekta nchini
yameongezeka kutoka asilimia 10 hadi asilimia 14 ambapo kwa sasa kuna mtrekta
16412.
Kwa upande wake Waziri
wa Kilimo, Chakula na Ushirika Stephen Wassira akimkaribisha Rais kuhutubia na
kufunga Maonesho ya Nane Nane Kitaifa alitoa wito kwa kanda zote nchini
kuendeleza mabanda yaliyopo katika viwanja wa maonesho ya wakulima nchi nzima
ili viwe shamba darasa na kwa kuwa na tija kwa wakulima na wafugaji.
Naye Mwenyekiti wa
Chama cha Kilimo Taifa (TASO) Englebert Moyo amewapongeza washiriki wote kwa
kuonesha teknolojia sahihi wakati wote wa maonesho inayowalenga wakulima na
wafugaji na ambayo wanaweza kuitumia katika mazingira yao.
Maonesho ya Nane Nane
nchini yameanzishwa rasmi mnano mwaka 1993 ambapo hadi sasa yanaendelea nchini
kupitia kanda ya Arusha, Dodoma, Morogoro, Mbeya na Mwanza na Lindi ambapo
maonesho hayo yanafanyika kitaifa kwa mara ya pili mfululizo na yanatarajiwa kuhitimishwa
2018 kwa kanda ya kusini baada ya kuongezewa miaka miwili ya kuwa wenyeji na
waandaji wa maonesho hayo kitaifa.
No comments:
Post a Comment