TANGAZO


Wednesday, August 5, 2015

Profesa Lipumba atuliza mzuka wa Wanachama CUF

*Aaghirisha kuzungumza na waandishi wa habari
*Wafuasi wafurika Makao Makuu
*Azungumza nao, awataka kukijenga Chama
*Wajikuta njia panda
Baadhi ya wanachama na wafuasi wa Chama cha Wananchi (CUF), wakiwa wamefurika Makao Makuu ya chama hicho, Buguruni, Dar es Salaam leo, wakionesha kumuunga mkono Mwenyekiti wao, Profesa Ibrahim Lipumba na kuwataka wale wanaomkwaza kufukuzwa mara moja kwenye chama ili mwenyekiti huyo, aendelee na umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa) wakati huu wa kuelekea uchaguzi Mkuu, mwezi Oktoba. (Picha zote na Kassim Mbarouk-www.bayana.blogspot.coma)
Naibu Katibu Mkuu wa CUF Bara, Magdalena Sakaya akizungumza na waandishi wa habari, wakati alipokuwa akiwaomba radhi waandishi wa habari na kuaghirisha mkutano ulioitishwa na Mwenyekiti wake, Profesa Ibrahim Lipumba kwa ajili ya kuongea nao. Katikati ni Naibu Mkurugenzi wa Habari na Mawasiliano wa CUF, Abdul Kambaya na kulia ni Ofisa Harakati na Matukio wa CUF, Nurdin Msati.
Naibu Mkurugenzi wa Habari na Mawasiliano wa CUF, Abdul Kambaya, akifafanua jambo kwa waandishi wa habari, wakati wa kuaghirishwa kwa mkutano wa Mwenyekiti wa CUF na waandishi wa habari, jijini Dar es Salaam leo. Kushoto ni  na kulia ni Ofisa Harakati na Matukio wa CUF, Nurdin Msati. Kushoto ni Naibu Katibu Mkuu wa CUF, Bara, Magdalena Sakaya  na kulia ni Ofisa Harakati na Matukio wa CUF, Nurdin Msati.
Mpiga picha wa Magazeti ya Uhuru na Mzalendo, Emmanuel Ndege, akisaidiwa na baadhi ya waandishi na wanachama wa CUF baada ya kukatwa na panga la feni, wakati akijitahidi kupata picha ya viongozi hao, wakati wakiaghirisha mkutano wa Profesa Lipumba na waandishi wa habari ofisini hapo leo. 
Baadhi ya wanachama na wafuasi wa Chama cha Wananchi (CUF), wakiwa wamefurika nje ya Makao Makuu ya chama hicho, Buguruni, Dar es Salaam leo, wakionesha kumuunga mkono Mwenyekiti wao, Profesa Ibrahim Lipumba, huku wakitaka kusikia msimamo wake kuhusu tetesi zilizosambaa za kutaka kuachia ngazi kukiongoza chama hicho.
Baadhi ya wanachama na wafuasi wa Chama cha Wananchi (CUF), wakiwa wamefurika nje ya Makao Makuu ya chama hicho, Buguruni, Dar es Salaam leo, wakionesha kumuunga mkono Mwenyekiti wao, Profesa Ibrahim Lipumba, huku wakitaka kusikia msimamo wake kuhusu tetesi zilizosambaa za kutaka kuachia ngazi kukiongoza chama hicho.
Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba, akizungumza na baadhi ya wanachama wa chama hicho, waliokusanyika Makao Makuu, Buguruni, Dar es Salaam leo, kutaka kujua kuhusu tetesi zilizozagaa katika mitandao ya kijamii, za kutaka kujiuzulu nafasi yake katika chama hicho.
Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba, akizungumza na baadhi ya wanachama wa chama hicho, waliokusanyika Makao Makuu, Buguruni, Dar es Salaam leo.
Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba, akizungumza na baadhi ya wanachama wa chama hicho, waliokusanyika Makao Makuu, Buguruni, Dar es Salaam leo, kutaka kujua kuhusu tetesi zilizozagaa katika mitandao ya kijamii, za kutaka kujiuzulu nafasi yake katika chama hicho.

Na Kassim Mbarouk-www.bayana.blogspot.com
HALI ya Sintofahamu imezidi kuongezeka ndani ya Chama cha Wananchi (CUF), baada ya Mwenyekiti wake Taifa, Profesa Ibrahim Lipumba kuzungumza na wanachama wakati akituliza jazba walizokuwa nazo, wakitaka kujua hatma ya kiongozi wao huyo baada ya tetesi zilizoenea kwenye mitandao ya kijamii nchini.

Profesa Lipumba, aliibuka kutoka ofisini, Makoa Makuu ya chama hicho, Buguruni, Dar es Salaam, alipokuwa akitaka kuzungumza na waandishi wa habari na hatimaye kuahirisha mazungumzo hayo baada ya kuvutwa na kutakiwa na wazee pamoja na viongozi wa dini kwa mazungumzo naye ofisini hapo leo.
Profesa Lipumba aliwataka wanachama na wafuasi wa chama hicho, kushikama na kuwa kitu kimoja kwa ajili ya kukijenga chama chao.

Alisema Chama ni taasisi sio mtu kwani hata yeye alipoingia katika chama hicho, aliingia kama mwanachama wa kawaida tu hadi akafikia hatua aliyonayo sasa, kuwa kiongozi mkuu wa chama hicho.

"Shikamaneni mukijenge chama cheni, Chama ni taasisi sio mtu," aliwaambia Profesa Lipumba na kuingia zake ndani ya jengo la Makao Makuu na kwenda kuendelea na kikao chake na wazee pamoja na viongozi wa dini.

Jana wakati wa Mkutano Mkuu wa moja ya Vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Profesa Lipumba, hakuweza kuhudhuria, jambo liliozuwa sintofahamu kwa wanachama pamoja na wananchi kujiuliza kulikoni, huku msaidizi wake, Makamu Mwenyekiti wa CUF, Zanzibar, Juma Duni Haji, akikabidhiwa kadi ya Chadema na kupitishwa kuwa Mgombea Mwenza wa mgombe wa Urais, Edward Lowassa katika mbio zake za urais wa Tanzania.

Pia kutambulishwa kwa Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif kuwa mgombea pekee wa ukawa kwa nafasi ya Urais wa Zanzibar.

Hali ya taharuki hiyo, ilichangiwa zaidi na mitandao ya kijamii ya mawasiliano pamoja na simu na moja ya magazeti kuandika kuwa Profesa Lipumba kuachia ngazo kwa sababu ya kutokubaliana na maamuzi yaliyopitishwa katika umoja huo.

Huku kukiwa na tetesi kuwa Mwenyekiti huyo ametofautiana na baadhi ya viongozi wa chama chake kutokana na kile kilichoelezwa kuwa ni kupinga kwa msaidizi wake wa Zanzibar, Juma Duni Haji kwenda Chadema na kufanywa Mgombea mwenza wa Edward Lowassa anayewania Urais wa Tanzania katika uchaguzi mkuu wa Oktoba 2015.

No comments:

Post a Comment