TANGAZO


Sunday, August 9, 2015

Mwanaharakati aliyepigwa risasi aondoka Burundi

Mwanaharakati aliyepigwa risasi aondoka Burundi
Mwanaharakati maarufu wa haki za kibinaadamu nchini Burundi aliyepigwa risasi na kujeruhiwa vibaya na watu waliokuwa katika pikipiki anaondoka nchini humo kuelekea nchini Ubeljiji.
Pierre Claver Mbonimpa aliyeshambuliwa katika mji mkuu wa Burundi, Bujumbura mapema wiki hii anaenda Ulaya kupokea matibabu.
Amekuwa mkosoaji mkubwa wa tangazo la rais Pierre Nkurunziza kuwania muhula wa tatu.
Hadi kufikia sasa haijajulikana ni nani aliyekuwa amelenga kumtoa uhai.
Amekuwa mkosoaji mkubwa wa tangazo la rais Pierre Nkurunziza
Katibu mkuu wa Umoja wa mataifa Ban Ki-moon alikuwa miongoni mwa viongozi wa kimataifa waliotaka uchunguzi wa kina ufanyike ilikubaini nani aliyemshambulia bwana Mbonimpa.
Shambulizi hilo lilifuatia lile la jumapili wiki iliyopita ambapo mshauri wa rais Nkurunziza, jenerali Adolphe Nshimirimana aliuawa katika shambulizi ndani ya gari lake mjini Bujumbura.
Wiki iliyopita Jenerali Adolphe Nshimirimana aliuawa katika shambulizi ndani ya gari lake mjini Bujumbura.
Alikuwa akisimamia usalama wa rais.
Burundi imekabiliwa na ghasia tangu hatua ya rais Nkurunziza mnamo mwezi Aprili kutaka kuwania muhula wa tatu.
Wapinzani wamedai kwamba hatua hiyo ni kinyume na katiba huku jaribio la mapinduzi likifeli mnamo mwezi Mei.
Uchaguzi wa urais ulifanyika mwezi uliopita ambapo bwana Nkurunziza alishinda lakini ulisusiwa na upinzani.

No comments:

Post a Comment