TANGAZO

Thursday, August 27, 2015

Moto wateketeza nyumba na familia ya watu 9 Buguruni Malapa jijini Dar es Salaam

Baadhi ya wananchi wakiwa kwenye nyumba iliyoteketea kwa moto Buguruni Malapa wakiangalia athari zilizopatikana katika ajali hiyo. Watu 9 wa familia ya Masoud Mattar, mmiliki wa nyumba hiyo, walipoteza maisha kwa kuteketea kwa moto huo. (Picha zote na Kassim Mbarouk-www.bayana.blogspot.com)
Baadhi ya wananchi wakiwa kwenye nyumba iliyoteketea kwa moto Buguruni Malapa wakiangalia athari zilizopatikana katika ajali hiyo. 
Baadhi ya wandishi wa habari na askari kazu wakipata picha ndani ya nyumba iliyoteketea kwa moto Buguruni Malapa leo. 
Baadhi ya wananchi wakiwa kwenye nyumba iliyoteketea kwa moto Buguruni Malapa jijini leo.
Baadhi ya Askari Polisi na askari kanzu wakiwa nje ya nyumba iliyoteketea kwa moto Buguruni Malapa jijini Dar es Salaam leo
Mbunge wa Ilala, Mussa Zungu, akizungumza na baadhi ya askari kazu waliokuwepo katika tukio hilo, Buguruni Malapa jijini jijini Dar es Salaam leo.  
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Sadiki (kushoto) na Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Raymond Mushi, wakiwasili kwenye nyumba iliyoteketea kwa moto, Buguruni Malapa jijini leo. 
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Sadiki akiangalia athari zilizopatikana katika ajali hiyo. 
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Sadiki (kulia) na Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Raymond Mushi (katikati), wakiangalia athari zilizopatikana katika ajali hiyo. Kushoto ni Mkuu wa Matukio wa Polisi Kanda maalumu ya Dar es Salaam, SSP Amani Makanyaga. 

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam , Said Sadiki (wa pili kulia), akipatiwa maelezo na Mkuu wa Matukio wa Polisi Kanda maalumu ya Dar es Salaam, SSP Amani Makanyaga, alipofika kwenye nyumba iliyoteketea kwa moto, Buguruni Malapa jijini leo. Kushoto ni Kamanda wa Polisi Kanda maalum ya Dar es Salaam, Kamishna Suleiman Kova. 
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam , Said Sadiki (wa pili kulia), akimweleza jambo Kamanda wa Polisi Kanda maalum ya Dar es Salaam, Kamishna Suleiman Kova, walipokuwa wakiangalia nyumba nyumba iliyoteketea kwa moto, Buguruni Malapa jijini leo. 
Baadhi ya vifaa vya matumizi ya nyumbani vikiwa vimeteketea katika nyumba hiyo. 
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Sadiki, akikagua nyumba iliyoteketea kwa moto. 
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Sadiki, akizungumza na waandishi wa habari nje ya nyumba iliyoteketea kwa moto na famila ya watu 9 ya Masoud Mattar kupoteza maisha katika ajali hiyo. 
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Sadiki (kulia), akimfariji baba wa familia iliyoteketea kwa moto, Masoud Mattar, wakati alipomtembelea baada ya nyumba yake pamoja na familia yake ya watu 9 kuteketea kwa moto, Buguruni Malapa usiku wa kuamkia leo. 
Baadhi ya miili ya watu tisa ya wana familia ya Masoud Mattar, iliyoteketea kwa moto, Buguruni Malapa ikiwa Msikiti wa Muhimbili kwa ajili ya kusaliwa tayari kwenda kuzikwa Makaburi ya Kisutu jijini Dar es Salaam leo. 

Waombolezaji wakiwa wameubeba mmoja wa miili 9 ya wana familia ya Masoud Mattar, iliyoteketea kwa moto, Buguruni Malapa, Dar es Salaam, wakati wa kwenda kuizika Makaburi ya Kisutu, jijini leo.  
Waombolezaji wakiwa wameubeba mmoja wa miili 9 ya wana familia ya Masoud Mattar, iliyoteketea kwa moto, Buguruni Malapa, Dar es Salaam, wakati wa kwenda kuizika Makaburi ya Kisutu, jijini leo.  
Waombolezaji wakiuzika mmoja wa mwili wa wanafamilia ya watu 9 ya Masoud Mattar, walioteketea kwa moto, Buguruni Malapa usiku wa kuamkia leo. 
Waombolezaji wakiuzika mmoja wa mwili wa wanafamilia ya watu 9 ya Masoud Mattar, walioteketea kwa moto, Buguruni Malapa usiku wa kuamkia leo. 
Mbunge wa Ilala, Mussa Zungu, akizungumza na waandishi wa habari wakati wa mazishi ya miili ya wanafamilia  9 ya Masoud Mattar, walioteketea kwa moto, Makaburi ya Kisutu jijini Dar es Salaam leo. 
Waombolezaji wakiomba dua baada ya kuizika miili ya wanafamilia ya watu 9 ya Masoud Mattar, walioteketea kwa moto, Makaburi ya Kisutu jijini Dar es Salaam leo.

No comments:

Post a Comment