TANGAZO


Thursday, August 27, 2015

Miili ya wahamiaji yapatikana Austria

Image copyright4 news
Image captionLori lililokuwa na miili ya wahamiaji
Maafisa wa serikali ya Austria wamesema kuwa wa wamegundua miilli ya wahamiaji kadhaa ambayo iliachwa ndani ya lori moja katika mkoa wa Burgenland, karibu na mpaka wa Hungary.
Polisi wanasema kuwa kulikuwa na kati ya miili 20 na 50 ndani ya jokovu ya gari hilo.
Waziri wa masuala ya ndani amesema tukio hilo linaashiria umuhimu wa suala la uhamiaji kushughulikiwa kwa dharura na viongozi wa Muungano wa Ulaya EU.
Miili hiyo imepatikana wakati viongozi wa Ujerumani ,Austria na nchi sita za mashariki mwa visiwa vya Balkan, wakikutana mjini Vienna kuzungumzia tatizo la uhamiaji.
Kansella wa Ujerumani Angela Merkel, amesema viongozi hao wamesikitishwa na ripoti hiyo.
Image copyright
Image captionKambi ya wahamiaji Austria
Amesema tukio hilo ni onyo kwa mataifa ya Ulaya kwamba swala la uhamiaji linaweza tu kutatuliwa iwapo kutakuwa na ushirikiano na uwajibikaji.
Nchi za ulaya zinazopokea idadi kubwa wahamiaji zimeonya kuwa iwapo nchi zingine hazitakubali kuwapa hifadhi wahamiaji athari za haua hiyo zitashuhudiwa katika Jumuiya nzima ya Ulaya.

No comments:

Post a Comment