Naibu rais wa shirikisho la riadha duniani IAAF, Lord Coe amekariri kuwa madai ya matumizi ya dawa za kusisimua misuli ni vita dhidi ya riadha na kuongeza kuwa ni wakati wa kujitokeza na kutetea mchezo huo.
Jarida la Sunday Times limechapisha majibu ya wanariadha 5,000 ambayo yamehushiwa wanariadha na udanganyifu wa hali ya juu na matumizi ya madawa ya kuongeza nguvu.
Shirikisho la riadha duniani IAAF limeeleza kuwa matokeo ya vipimo vya damu sio ithibati tosha ya utumiaji wa dawa hizo.
‘’Ni vita dhidi yamchezo huu. Hakuna chochote katika historia yetu ya ushindani bora na uadilifu katika ukaguzi kinachostahili uvamizi wa aina hii’’. Alieleza.
Gazeti la Sunday Times na runinga ya Ujerumani ARD/WDR vilichunguza matokeo ya ukaguzi wa damu 12,000 uliyofanywa kati ya mwaka wa 2001-2012.
Aidha vyombo hivyo viliwatumia wataalam dhidi ya utumiaji wa dawa za kuongeza nguvu wakiwemo wanasayansi, Robin Parisotto na Michael Ashenden, ambao wamesema
kuwa majibu hayo licha ya kutoonyesha uwezekano wa matumizi ya dawa hizo, yanatiliwa shaka.
Vyombo hivyo viliripoti majibu ya zaidi ya wanariadha 800, thuluthi moja wakiwemo mabingwa wa mbio za Olimpiki na mashindano ya riadha duniani, yalitiwa shaka kwani hayakufutiliwa.
Kwenye taarifa yake, IAAF, imepinga vikali madai hayo.
Coe, anayewania urais kwenye uchaguzi wa shirikisho la IAAF utakaofanyika tarehe 19 Agosti, ameongeza kuwa,
'Matumizi ya rekodi zetu, licha ya njia zilizotumika kupokea, imeonyesha ujangili wa hali ya juu'.
No comments:
Post a Comment