TANGAZO


Thursday, August 27, 2015

Asbel Kiprop kutetea taji lake Beijing

Image captionAsbel Kiprop
Mashindano ya riadha yaendelea Beijing, huku wanariadha wa Kenya wakifuzu kwa fainali.
Katika mbio za mita 1500, bingwa mtetezi Asbel Kiprop alifuzu kwa fainali na kuimarisha matumaini ya kuhifadhi taje lake.
Wakenya wengine waliofuzu ni Silas Kiplagat, Elijah Motonei Manangoi na Timothy Cheruiyot
Wanariadha wengine wa Africa waliofuzu kwa fainali ni pamoja na
  • Bingwa wa Olimpiki Taoufik Makhloufi wa Algeria
  • Wanariadha wa Ethiopia Mekonnen Gebremedhin na Aman Wote
  • Kutoka Morocco's Yssine Bensghir na Abdalaati Iguider
  • Djibouti ni Abdi Waiss Mouhyadin
  • Afrika Kusini nayo itawakilishwa na Johan Cronje

No comments:

Post a Comment