TANGAZO


Tuesday, July 7, 2015

Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na michezo yahitimisha mafunzo kwa kutembelea miradi mbalimbali Wilaya ya Nzega

Mwenyekiti wa Kikundi cha Tujiajiri Group cha Tarafa ya Nyasa wilaya ya Nzega Bw. Fanuel Kifunyu (waKwanza kulia)akiongea na kuonyesha ujumbe kutoka Wizara ya Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo kuhusu Bidhaa mbalimbali wanazotengeneza zikiwamo Sabuni, matofali ya kufungamana na karanga baada ya kupata mafunzo ya mfuko wa Maendeleo ya Vijana, Stadi za Maisha, Ujasiriamali na Uongozi Bora. Wengine pichani ni Afisa Vijana Laurean Masele (wa pili kutoka kulia), Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Maendeleo ya Vijana Uratibu na Uhamasishaji (katikati) na Afisa Vijana Amina Sanga (Mwenye kiremba cha Njano. 
Mkuu wa Kituo cha Vijana Sasanda Bw.Laurean Masele (wa pili kutoka kulia) akichukua maelezo mbalimbali kutoka kwa Mwenyekiti wa Kikundi cha UWAVIMA (umoja wa wauza vifaa vya Ndani) Bw. Abdallah Mtutui juu ya mradi wao na maendeleo yake kwa ujumla.Kikundi hicho kimehudhuria Mafunzo ya Mfuko wa Maendeleo ya Vijana, Ujasiriamali, Uongozi Bora na Stadi za Maisha yanatolewa na Wizara ya Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo wilayani Nzega. 
Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Maendeleo ya Vijana Uratibu na Uhamasishaji Bi.Esther Riwa(wa Kwanza kushoto) akipita katika shamba la nyanya la kikundi cha Nserema kinacholima Nyanya, Matikiti na Kabeji kutoka  kijiji cha Iyombo Tarafa ya Nyasa. Kikundi icho kinategemea kuomba mkopo kupitia Mfuko wa Maendeleo ya Vijana ili kuboresha kilimo chao kwa kununua pembejeo za kilimo,kununua mbegu bora na madawa ya kuulia wadudu.katikati mwenye shatu jekundu ni Mwenyekiti wa kikundi icho Bw. Stephen Ndikamara.

No comments:

Post a Comment