TANGAZO


Sunday, July 26, 2015

Warsha kwa wajumbe wa Kamati ya Maafa ya Wilaya ya Mkoani Kisiwani Pemba

Mkurugenzi wa Idara ya Maafa Zanzibar Ali Juma Hamad, akizungumza na wajumbe wa kamati ya maafa Wilaya ya Mkoani pamoja na walimu wa skuli za sekondari na msingi Wilaya hiyo, huko katika ofisi ya Mkuu wa Wilaya Mkoani.
Wajumbe wa Kamati ya Maafa ya Wilaya ya Mkoani, pamoja na walimu wa skuli za sekondari na Msingi Wilayani humo, wakimsikiliza kwa makini Mkurugenzi wa Idara ya Maafa Zanzibar ambae hayupo pichani wakati alipokuwa akifungua warsha ya siku mbili.
Ofisa Elimu Wilaya ya Mkoani, Kisiwani Pemba Seif Mohamed Seif, akichangia mada ya sheria ya kupunguza na kukabiliana na maafa Zanzibar na mambo mengine, wakati wa kongamano la maafa kwa wajumbe wa kamati ya kukabiliana na maaafa wilaya ya Mkoani, walimu wa skuli za Sekondari na Wilaya hiyo huko Mkoani.
Ofisa Mipango Wilaya ya Mkoani Mwalim Omar Shehe Omar, akitoa ufafanuzi juu ya Wilaya kutakiwa kuwa na bajeti maalumu ya kukabiliana na maafa pale yanapotokea.
Mkurugenzi wa Idara ya Maafa Zanzibar Ali Juma Hamad, akitoa ufafanuzi wa Maswali mbali mbali yaliyoulizwa na wajumbe wa kamati ya kukabiliana na Maafa Wilaya Mkoani na Walimu wa skuli za Sekondari na Msingi Wilaya ya Mkoani.

Mkufunzi wa mada ya sheria ya kupunguza na kukabiliana na maafa Zanzibar, Amina Talib akiwasilisha mada hiyo kwa wajumbe wa kamati za kukabiliana na maafa Wilaya ya Mkoani na Walimu wa skuli za Sekondani na Msingi wilaya hiyo. (Picha zote na Abdi Suleiman, PEMBA.)

No comments:

Post a Comment