Mkurugenzi wa Kitengo cha Ubora wa Huduma za Afya Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Ali Mohamed Ali (kulia), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Dar es Salaam leo, wakati akitoa tamko kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dk. Donan Mmbando katika uzinduzi wa kampeni ya awamu ya pili ya wazazi nipendeni uliofanyika Dar es Salaam. Kutoka kushoto ni Kaimu Mkurugenzi Msaidizi Kitengo cha Afya ya Uzazi na Mtoto Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Dk.Georgina Msemo na Mshauri wa Kiufundi wa Malaria kutoka Shirika la Marekani la Maendeleo ya Kimataifa (USAID)
Ofisa Uzazi Salama, Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Dk.Heavengton Mshiu (kulia), akizungumza katika uzinduzi huo.
Mshauri wa Masuala ya Afya ya Uzazi wa Taasisi ya Center for Comminication Programs Johnns HopKins University, Dk,.Rosemarie Madinda (kulia), akizungumza katika uzinduzi huo. Taasisi hiyo ndiyo inayoendesha kampeni hiyo.
Kaimu Mkurugenzi Msaidizi Kitengo cha Afya ya Uzazi na Mtoto Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Dk.Georgina Msemo (kulia), akizungumza kwenye uzinduzi huo.
Mwongozaji wa uzinduzi huo akiendelea na kazi.
Ofisa Uzazi Salama, Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Heavengton Mshiu (kushoto), akimpongeza Mkurugenzi wa Kitengo cha Ubora wa Huduma za Afya Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Ali Mohamed Ali, baada ya kutoa tamko la Wizara hiyo katika uzinduzi huo.
Mwanamuziki Nyoshi Al-Saadat wa Bendi ya Muziki wa Dansi ya FM Academia "Wana wa Ngwasuma" itakayotoa burudani katika maonyesho mbalimbali yatakayokwenda sanjari na uzinduzi huo yatakayofanyika kuanzia kesho viwanja vya Mwembe Yanga Temeke Dar es Salaam kuanzia kesho, akizungumza katika uzinduzi huo utakaopambwa na burudani za kumwaga.
Na Dotto Mwaibale
SERIKALI imesema imepiga hatua katika kupunguza vifo vya watoto waliochini ya miaka mitano toka 157 mwaka 1990 hadi kufikia 54 kwa mwaka 2013.
Hayo yalibainishwa na Mkurugenzi wa Kitengo cha Ubora wa Huduma za Afya Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Ali Mohamed Ali wakati akitoa tamko kwa niaba ya Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dk. Donan Mmbando katika uzinduzi wa kampeni ya awamu ya pili ya wazazi nipendeni uliofanyika Dar es Salaam leo.
Alisema kati yua watoto hai 1,000 wanaozaliwa na kufikia lengo la Melenia (MDG) 4 waliojiwekea kufikia mwisho wa mwaka huu Disemba 2015.
"Pamoja na mafanikio hayo bado hari si shwari kwa upande wa vifo vinavyotokana na uzazi kwani vimepungua kutoka 770 mwaka 1990 na kufikia 410 kwa mwaka 2014 kwa kila vizazi hai 100,000 tofauti na lengo tulilojiwekea kufikia Disema 2015 kuwa vipungue kufikia 193 kwa kila vizazi hai 100,000" alisema Dk.Ali.
Alisema Kampeni ya Wazazi Nipendeni awamu ya kwanza ilitengenezwa na Serikali ya Tanzania kupitia Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii kwa kushirikiana na msaada toka watu wa Marekani kupitia taasisi ya USAID, Mfuko wa Malaria wa Rais wa Marekani na taasisi ya Kukinga na kuzuia Magonjwa.
Dk. Ali alisema programu hiyo ilihusisha kutuma ujumbe uliolenga kuimarisha afya ya mjamzito na mtoto na kuwa ilizinduliwa hapa nchini jijini Mwanza kwa mara ya kwanza mwezi Novemba, 2012.
Alisema katika kampeni hiyo ya masuala ya afya na ustawi wa jamii vyombo vyote vya habari ni muhimu zaidi kuhabarisha na kuwa ujumbe mfupi wa simu za kiganjani wenye taarifa anwai zitakuwa zinatumwa wakati wowote wa ujauzito mpaka mwaka mmoja baada ya kujifungua.
Aliongeza kuwa ili kujiunga mhusika, ndugu, jirani au rafiki atatuma ujumbe "mtoto" kwenda namba 15001 jambo litakalosaidia kupunguza vifo vitokanavyo na uzazi, mtoto mchanga na mtoto alie chini ya miaka mitano.
Alisema uzinduzi wa kampeni hiyo unakwenda sanjari na maonyesho mbalimbali, upimaji wa damu, masuala ya huduma ya VVU na Ukimwi yatakayoanza leo asubuhi viwanja vya Mwembe Yanga Temeke jijini Dar es Salaam.
Dk. Ali alitumia fursa hiyo kuwakaribisha wananchi wa mkoa wa Dar es Salaam na mingine hasa wanaume na wanawake kufika kwenye maonyesho hayo kupata huduma za afya ya uzazi ambayo yataambatana na burudani za muziki kutoka bendi za Wanaume Familia, Ngwasuma, Wanaume Halisi na nyingine nyingi.(Imeandaliwa na Dotto Mwaibale)
No comments:
Post a Comment