Katika kuimarisha ulinzi wakati huu ambao vikao vya Chama Cha Mapinduzi (CCM), vikiendelea Mjini Dodoma, jeshi la Polisi limeimarisha ulinzi katika mitaa mbalimbali, ikiwemo Barabara zinazolizunguka jengo la Makao Makuu ya chama hicho. (Picha zote na John Banda)
Polisi wakiwa katika lindo nje ya Ofisi ya Makao Makuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mjini Dodoma leo. Wajasiriamali wakiwa wamepanga nguo na bidhaa za aina mbalimbali wakisubiri wateja katika uzio wote unaozunguka jango la Makao Makuu ya Chama hicho, wakati huu ambao vikao vya chama hicho vikiendelea mjini Dodoma.
Farasi wa ulinzi akipita mbele ya wajasiriamali waliokuwa wamepanga nguo na bidhaa za aina mbalimbali huku wakisubiri wateja katika uzio unaozunguka jango la Makao Makuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), kipindi hiki cha kumpata mgombea wa nafasi ya Urais wa chama hicho, mjini Dodoma leo.
Askari wa Farasi akipita nje ya Jengo la Makao Makuu ya CCM, Mjini Dodoma leo.
Usafi ukiendelea kwenye Mitaa ya Mji wa Dodoma leo.
Juu na Chini: Usafi ukiendelea kwenye Mitaa ya Mji wa Dodoma leo.
Wafanyakazi wa Halmashauri ya Manispaa ya Dodoma wakifyagia Barabara ya Sita iliyopo nyuma ya jengo la Makao Makuu ya CCM, ambapo uongozi wa mji wa Dodoma upo katika maandalizi ya kupokea wageni wengi wanaoingia mjini humo kwa ajili ya Mkutano Mkuu wa chama hicho, unaotarajiwa kufanyika Julai 11 mwaka huu.

No comments:
Post a Comment