Waziri Mkuu wa Ethiopia na Mwenyekiti wa Viongozi wa Afrika katika Mapambano dhidi ya Malaria Mh.Hailemariam Dessalegn akiongea wakati wa hafla ya uzinduzi wa kiwanda cha kuzalisha viuadudu vya kuua viluwiluwi vya mbu wanaoeneza malaria ambapo aliipongeza serikali ya Tanzania katika kutekeleza Mradi huo utakaosaidia katika kupambana na vita dhidi ya malaria nchini Tanzania na Afrika kwa Ujumla, leo Mjini Kibaha.
Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Maendeleo laTaifa (NDC) Dkt. Chrisant Mzindakaya akiongea wakati wa hafla ya uzinduzi wa kiwanda cha kuzalisha viuadudu vya kuua viluwiluwi vya mbu wanaoeneza malaria na kupongeza jitihada za Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete katika kusimamia utekelezaji wa kiwanda hicho cha kuzalisha viuadudu vya kuua viluwiluwi vya mbu wanaoeneza malaria ili kutekeleza ahadi yake ya kutokomeza malaria nchini, leo Mjini Kibaha.
Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo akiongea wakati wa hafla ya uzinduzi wa kiwanda cha kuzalisha viuadudu vya kuua viluwiluwi vya mbu wanaoeneza malaria ambapo alishukuru na kupongeza uzinduzi wa kiwanda hicho kwani kitakuwa ni mwarobaini katika mapambano dhidi ya malaria kwa mkoa wa pwani na afrika kwa ujumla,leo Mjini Kibaha.
Waziri wa Viwanda na Biashara Mh. Abdalah Kigoda akiongea katika hafla ya uzinduzi wa kiwanda cha kuzalisha viuadudu vya kuua viluwiluwi vya mbu wanaoeneza malaria na kuahidi kushirikiana kwa karibu na shirika la maendeleo ya taifa (NDC) katika kutekeleza majukumu ya kiwanda hicho ili kutekeleza agizo la Rais Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete katika vita dhidi ya malaria kupitia Mradi huo, leo Mkoani Pwani.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete akimkabidhi zawadi Waziri Mkuu wa Ethiopia na Mwenyekiti wa Viongozi wa Afrika katika Mapambano dhidi ya Malaria Mh.Hailemariam Dessalegn wakati wa hafla ya uzinduzi wa kiwanda cha kuzalisha viuadudu vya kuua viluwiluwi vya mbu wanaoeneza malaria leo mkoani Pwani.
Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Maendeleo laTaifa (NDC) Dkt. Chrisant Mzindakaya akimkabidhi zawadi Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete wakati wa hafla ya uzinduzi wa kiwanda cha kuzalisha viuadudu vya kuua viluwiluwi vya mbu wanaoeneza malaria leo mkoani Pwani.
Waziri Mkuu wa Ethiopia na Mwenyekiti wa Viongozi wa Afrika katika Mapambano dhidi ya Malaria Mh. Hailemariam Dessalegn na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete wakifungua jiwe la msingi wakati wa hafla ya uzinduzi wa kiwanda cha kuzalisha viuadudu vya kuua viluwiluwi vya mbu wanaoeneza malaria leo mkoani Pwani.
Waziri Mkuu wa Ethiopia na Mwenyekiti wa Viongozi wa Afrika katika Mapambano dhidi ya Malaria Mh.Hailemariam Dessalegn na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete wakikata utepe kuashiria uzinduzi wa kiwanda cha kuzalisha viuadudu vya kuua viluwiluwi vya mbu wanaoeneza malaria, leo mkoani Pwani.
Waziri Mkuu wa Ethiopia na Mwenyekiti wa Viongozi wa Afrika katika Mapambano dhidi ya Malaria Mh. Hailemariam Dessalegn na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi mbalimbali waliohudhuria hafla hiyo, leo mkoani Pwani.
Waziri Mkuu wa Ethiopia na Mwenyekiti wa Viongozi wa Afrika katika Mapambano dhidi ya Malaria Mh. Hailemariam Dessalegn akisalimiana na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Mizengo Pinda wakati wa Halfa ya uzinduzi wa kiwanda cha kuzalisha viuadudu vya kuua viluwiluwi vya mbu wanaoeneza malaria, leo mkoani Pwani, Kushoto ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh. Mizengo Pinda akisalimiana na Mwenyekiti wa Bodi ya Shirika la Maendeleo laTaifa (NDC) Dkt. Chrisant Mzindakaya wakati wa Halfa ya uzinduzi wa kiwanda cha kuzalisha viuadudu vya kuua viluwiluwi vya mbu wanaoeneza malaria, leo mkoani Pwani,katikati ni Waziri wa Viwanda na Biashara Mh. Abdalah Kigoda.
Balozi
wa Cuba nchini Tanzania Bw. Jorge Luis Lopez akiongea wakati wa hafla ya
uzinduzi wa kiwanda cha kuzalisha viuadudu vya kuua viluwiluwi vya mbu
wanaoeneza malaria kilichojengwa kwa ushirikiano wa serikali ya Cuba na
Tanzania, ambapo aliahidi kuendelea kushirikiana na Serikali katika masuala
balimbali ya maendeleo leo mkoani Pwani. (Picha zote na Hassan Silayo-Maelezo)
Na
Benedict Liwenga-Maelezo
02/07/2015
02/07/2015
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete
amefurahishwa na uzinduzi wa Kiwanda cha kuzalisha viuadudu vya kuua viluwiluwi
vya mbu wanaoeneza ugonjwa wa malaria kilichopo eneo la viwanda, Tamco-Kibaha
mkoani Pwani ikiwa ni moja ya mikakati ya Serikali iliyojipangia ya kupambana
na kupunguza vifo visababishwavyo na ugonjwa huo.
Uzinduzi
huo ulifanywa na mgeni rasmi ambaye ni Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Kidemokrasia
ya Ethiopia, Mhe. Hailemariam Desalegn ambaye pia ni Mwenyekiti wa Umoja wa
Nchi zinazopambana na Malaria (ALMA).
Katika
uzinduzi huo, Rais Kikwete ameishukuru nchi ya Cuba kwani wao ndiyo walikubali
kutoa wataalamu pamoja na teknolojia ili kuisaidia Tanzania kuendeleza sekta ya
madawa ikiwemo kupambana dhidi ya ugonjwa wa malaria pamoja na kuwafundisha
wataalamu wa Tanzania ili waweze kuendeleza kiwanda hicho.
Rais
Kikwete alieleza kwamba, akiwa nchini Cuba mnamo Novemba 2009 alitembelea
viwanda vya kuzalisha bidhaa mbalimbali za kibaiolojia kikiwemo kiwanda cha
Biolarvicides cha LABIOFAM SA kinachomilikiwa na Serikali ya Cuba hivyo
Serikali hiyo ilipokubali awamu ya kwanza ilipanga kujenga kiwanda cha
Biolarvicides kwa lengo la kuua viluwiluwi wa mbu wanaoeneza malaria ambapo
mradi huo ndo umezinduliwa rasmi tarehe 2 Julai mwaka huu na pia katika awamu
ya pili ilikuwa ni ujenzi wa viwanda vya kuzalisha dawa mbalimbali kwa ajili ya
kutibu na kuzuia magonjwa ya binadamu na wanyama na mwisho ni awamu ya tatu ya
ujenzi wa viwanda vya dawa na vyakula vya ziada yaani Food supplement kwa ajili
ya watu wenye magonjwa ya kudumu na kuzalisha mbolea za kibaiolojia
(bio-fertilizers).
"Chimbuka
la ujenzi wa kiwanda hiki ni ziara yangu niliyoifanya nchini Cuba, ndipo
niliona kuna umuhimu wa kuiomba Serikali ya Cuba itusaidie kutupatia teknolojia
pamoja na wataalamu lakini pia niliagiza Shirika la Maendeleo la Taifa (NDC)
wajenge ushirikiano kwa ajili ya kutengeneza kiwanda nchini Kwetu na matokeo
yake ndo haya", alisema Dkt. Kikwete.
Rais
Kikwete alimshukuru Balozi wa Cuba nchini Tanzania, Balozi Jorge Luis Lopez kwa
ushirikiano mkubwa aliouonyesha kwa kuisaidia Tanzania katika kuhakikisha
kwamba kiwanda hicho kinawepo nchini na kwa ukarimu wao pasipo tamaa ya kutoa
teknolojia hiyo, licha ya nchi yao kutakuwa tajiri wao walitupati teknolojia
hii na walishirikiana nasi katika ujenzi wa kiwanda hicho pamoja na wataalamu
"Huu
ndiyo urafiki wa kweli na udugu nakuomba Balozi unifikishie salamu zangu za
dhati na shukurani zangu mimi pamoja na watanzania wote kwa ajumla kwa Rais
Raul Castro kwa mchango wake mkubwa kwa nchi yetu Tanzania", Alisema Dkt.
kikwete.
Naye
Balozi wa Cuba nchini Tanzania, Balozi Jorge Luis Lopez ameziomba nchini
nyingine ziweze kuiga ushirikiano mkubwa wa Serikali ya Tanzania na Cuba na pia
kwa niaba ya Serikali yake amemshukuru Rais Kikwete kwa utendaji kazi wake
mzuri, uhusiano mzuri ambao ameujenga na kati ya Tanzania na Cuba.
Naye
mgeni rasmi Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Ethiopia na Mwenyekiti wa
Umoja wa Nchi zinazopambana na Malaria (ALMA) na ametoa pongezi zake za dhati
na kueleza kwamba, hiyo ni hatua nzuri na kusema kuwa kushuka kwa idadi ya vifo
nchini Tanzania ni ishara ya uongozi mzuri na bora wa Rais Kikwete na ishara
nzuri kwa kuiacha nzuri katika mahali pazuri pamoja mahali pazuri dhidi ya
umaskini
Aidha,
ameeleza kuwa uwepo wa kiwanda hiko itakuwa ni ishara nzuri ya mapambano na
yeye kama Mwenyekiti wa Umoja wa nchi zinazopambana (ALMA) dhidi ya malaria
atazihamasisha nchi nyingine kutumia Afrika waweze kutumia mazao yatokanayo na
kiwanda hicho.
Kampuni
ya Tanzania Biotech Products Limited ni Kampuni iliyoundwa kwa ajili ya
kuendesha Kiwanda cha kuzalisha Viuadudu vya kuua Viluwiluwi vya mbu wanaoeneza
malaria kilichopo Kibaha, Pwani ambacho kimejengwa kwa kushirikiana na Kampuni
ya LABIOFAM SA ya Cuba a kiwanda hiki kinatokana na agizo l Rais Kikwete
alilolito Januari 4 , 2010 kwa shirika la Taifa la Maendeleo (NDC) baada ya
ziara yake nchini Cuba.














No comments:
Post a Comment