Baadhi ya wanakikundi cha Mkombozi kata ya Masanga wilayani Kishapu Shinyanga, wakiwa na mbuzi waliowapata kutoka Idara ya Uratibu Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu kupitia Mradi wa kupunguza Athari za Maafa ya Ukame tarehe 5 Julai, 2015, Mradi huo unafadhiliwa na Benki ya Dunia kupitia UNICEF.
Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, Regina Kikuli (wa kwanza kushoto) akimsikiliza mwanakikundi cha Mkombozi kata ya Masanga wilayani Kishapu Shinyanga wakati akieleza manufaa ya ufugaji wa mbuzi waliowapata kutoka Idara ya Uratibu Maafa Ofisi ya Waziri Mkuu kupitia Mradi wa kupunguza Athari za Maafa ya Ukame wilayani Kishapu Shinyanga, tarehe 5 Julai, 2015, Mradi huo unafadhiliwa na Benki ya Dunia kupitia UNICEF. Kulia kwake ni Mkurugenzi Idara ya Uratibu Maafa Ofisi hiyo, Brigedia Jenerali, Mbazi Msuya.
No comments:
Post a Comment