Baadhi ya wanachama wa Chama cha Mapinduzi wakifuatilia mkutano huo uliofanyika Afisi Kuu ya CCM Kisiwandui Mjini Zanzibar.
Baadhi ya wanachama wa Chama cha Mapinduzi wakifuatilia mkutano huo uliofanyika Afisi Kuu ya CCM Kisiwandui Mjini Zanzibar.
Mwenyekiti wa CCM Mkoa Mjini, Borafia Silima akitoa ufafanuzi katika mkutano uliohudhuriwa na wajumbe wa ngazi mbali mbali za Chama na waandishi wa Habari Afisi kuu ya CCM Kisiwandui Mjini Zanzibar.
Na Mwashungi Tahir/Maryam Kidiko
-Maelezo Zanzibar 31/07/2015
CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimesema
ni Chama kikubwa chenye wafuasi na wanachama wengi pamoja
na Viongozi wenye hekima, busara, mapenzi na uadilifu mkubwa.
Hayo yameelezwa na Katibu wa
CCM Mkoa Mjini Mohammed Omar Nyawenga wakati alipokuwa akitoa taarifa
kwa Waandishi wa Habari kuhusu kujitoa Chama cha Mapinduzi Waziri
Mkuu wa zamani Edward Ngoyai Lowassa na kujiunga na Chama cha upinzani
huko Afisi Kuu ya CCM Kisiwandui
Amesema CCM ni Chama kinacho
aminiwa na kukubalika na Wananchi wengi wa Tanzania hivyo kujitoa
kwa mwanachama mmoja ama kikundi cha wanachama haiwezi kukiathiri chama
hicho.
Nyawenga ameongeza kuwa wingi wa
wanachama wa chama hicho haujaletwa na utajiri wa vingozi wake bali
umetokana na uimara wa Siasa, Sera na itikadi yake.
Alisema CCM haina hasara kumpoteza
mwanacham mmoja anaetaka kubadili sera na itikadi ya Chama kwa maslahi
yake binafsi na marafiki zake hata kama utajiri wake ni mkubwa wa
kupindukia.
Ameongeza kuwa uwamuzi wa Lowassa
kujiondowa ndani ya Chama hicho sijambo la kukishituwa chama, viongozi, pamoja
na wanachama wake na hakiwezi kudhoofika wala kutetereka.
Alisema hii sio mara ya kwanzi kwa
Chama cha Mapinduzi kuondokewa na kiongozi mwandamizi na kujiunga
na vyama vya upinzani na bado kinaendelea kuimarika.
“Mwaka 1989, CCM iliwafukuza
uanachama viongozi waandamizi 11 akiwemo Waziri Kiongozi mstaafu wa Zanzibar
Seif Sharif Hamad, akafuatia Agostino Lyatonga Mrema na mwaka jana CCM
ilimfukuza uanachama aliyekua Mwakilishi wa Kiembesamaki Mansour Yussf,”
alikumbusha Katibu wa Chama Mkoa.
Nyawenga aliweka wazi kuwa
umaarufu alionao Lowassa inawezekana umejengwa kutokana na CCM lakini
haiwezekani umaarufu wa Chama hicho umejengwa kutokana na yeye.
Alisema wanachama wa Zanzibar
waliokuwa wakimuunga mkono Lowassa katika azma ya kuomba kuteuliwa
na CCM kuwa mgombea wa kiti cha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
walifanya hivyo kwa sababu ya siasa, sera na ilani ya Chama na sasa baada
ya kuhama wameamua kujitenga na hawako pamoja naye.
Mwenyekiti wa Mkoa wa Mjini Magharib
Borafia Silima amesema kwamba Tanzania inaheshimika kuwa ni nchi
yeye amani, na mshikamano na Chama cha Mapinduzi kinafuata utaratibu wa
katiba iliyowekwa.
Amesema kila Mwanachama anayo haki
na uhuru wa kuchaguwa kiongozi anayemtaka na yeye kuchaguliwa na
mtu yeyote ikiwa ni Demokrasia iliyotandikwa na Chama hicho
No comments:
Post a Comment