TANGAZO


Sunday, July 5, 2015

Mkurugenzi wa Msama Promotions asaidia vituo vya kulelea yatima jijini Dar es Salaam

Mkurugenzi wa Msama Promotion, Alex Msama akizungumza na waandishi wa habari, wakati alipokabidhi misaada ya vitu mbalimbali, vikiwemo vyakula, mafuta ya kula, kujipaka na sabuni kwa vituo vya yatima mbalimbali jijini Dar es Salaam leo, ikiwa ni sehemu ya fedha zilizopatikana katika tamasha la Pasaka. (Picha zote na Kassim Mbarouk-www.bayana.blogspot.com)
Mkurugenzi wa Msama Promotion, Alex Msama (kulia), akimkabidhi moja ya mfuko wa unga wa ngano Katibu wa Kituo cha Yatima cha Chakuwama cha Sinza, Ally Said kwa ajili ya kituo hicho, jijini Dar es Salaam leo, ikiwa ni sehemu ya fedha zilizopatikana katika tamasha la Pasaka.  
Mkurugenzi wa Msama Promotion, Alex Msama (kulia), akimkabidhi vitu mbalimbali Halima Ramadhan wa Kituo cha Yatima cha Mwandaliwa cha Boko jijini Dar es Salaam leo.
Mkurugenzi wa Msama Promotion, Alex Msama akimkabidhi mtoto Gatson Edwin (kushoto) wa Kituo cha yatima cha Honoratha, Temeke Dar es Salaam, mafuta ya kujipaka na katuni ya sabuni ya kufulia ikiwa ni baadhi ya vitu mbalimbali alivyokabidhi kwa vikundi mbalimbali vya yatima na wanaoishi katika mazingira magumu, jijini leo, ambavyo ni sehemu ya fedha zilizopatikana katika tamasha la Pasaka. Aliyembeba ni dada wa Edwin, Gatson Edwin.
Mkurugenzi wa Msama Promotion, Alex Msama akimkabidhi mtoto Ridhwan Yussuf wa Kituo cha yatima cha Almadina Children Home cha jijini Dar es Salaam. Katikati ni mtoto Rama Abdul wa kituo hicho.
Mkurugenzi wa Msama Promotion, Alex Msama (kulia), akimkabidhi yatima Kheri Suleiman wa Kituo cha Umra cha Magomeni jijini Dar es Salaam mafuta ya kujipaka pamoja na vitu mbalimbali, vikiwemo vyakula, mafuta na sabuni. 
Mkurugenzi wa Msama Promotion, Alex Msama (kulia), akimkabidhi yatima Shaaban Muzamil wa Kituo cha Umra cha Magomeni jijini Dar es Salaam ndoo ya mafuta ya kula pamoja na vitu mbalimbali, vikiwemo vyakula, mafuta na sabuni. 
Mkurugenzi wa Msama Promotion, Alex Msama (katikati), akipiga picha na yatima wa vituo vya Malezi Kids na Arrahaman vya jijini mara baada ya kukabidhi vitu mbalimbali, vikiwemo vyakula, mafuta na sabuni.  
Mkurugenzi wa Msama Promotion, Alex Msama akizungumza na vijana wa vituo hivyo.

No comments:

Post a Comment