TANGAZO


Friday, July 3, 2015

Kipindupindu chawaua watu 29 Sudan Kusini

Kipindupindu
Watu 29 wamefariki kutokana na mlipuko wa ugonjwa wa kipundupindu nchini Sudan Kusini huku wengine 1000 wakiwa katika hatari ya maambukizi kulingana na Umoja wa mataifa.
Takriban visa 484 vya ugonjwa huo ikiwemo vifo 29 , sita kati yake ikiwa ni vya watoto wa chini ya umri wa miaka mitano,vimeripotiwa kufikia mwishoni mwa mwezi Juni kulingana na afsi ya mratibu wa maswala ya kibinaadamu katika umoja wa kimataifa.
Kwa mujibu wa ripoti hiyo, watoto elfu tano walio chini ya umri wa miaka mitano, wako hatarini ya kufa kutokana na ugonjwa huo, ikiwa hatua za dharura hazitachukuliwa.
null
Kipundupindu
Ugojwa huo ni hatari zaidi hasa miongoni mwa watoto kwa sababu husababisha mwili kupoteza maji mengi kutokana na kutapika na kuendesha.
Shirika la afya duniani WHO, na wasaidizi wanafanya juhudi za kuwahamasisha watu kuhusu jinsi ya kuzuia ugonjwa huo na pia kutoa chanjo.
Wizara ya afya wa Sudan Kusini ilitangaza mlipuko wa ugonjwa huo tarehe 23 mwezi uliopita, wakati watu kumi na nane walipopoteza maisha yao.
Inaaminika kuwa ugonjwa huo ulianza Juni katika kambi za shirika la Umoja wa mataifa UN, mjini Juba kabla ya kusambaa katika maeneo mengine ya mji huo.
null
Kipindupindu
Mwaka uliopita, takriban watu mia moja sitini na saba walifariki kutokana na kipindupindu nchini humo kabla ugonjwa huo kudhibitiwa.
Kutokomeza ugonjwa huu, unaosambaa kutokana na matumizi ya maji machafu na chakula kilchochanganyika na uchafu wa kinyesi , imekua changamoto kubwa kwa serikali ya sudan kusini na wafanyakazi wa kutoa misaada.
Umoja wa mataifa unakadiria kuwa zaidi ya raia wa Sudan Kusini milioni nne nukta tano wanakabiliwa na tishio la baa la njaa.
Kufikia sasa visa vya ugonjwa huo vimeripotiwa mjini Juba lakini madaktari wanafanya uchunguzi zaidi kuhusiana na visa vingine sita ambavyo vimeripotiwa nje ya mji huo.
null
Kipindupindu
Vita vya wenyewe kwa wenyewe nchini Sudan kusini vilianza Disemba mwaka wa 2013 baada ya rais Salva Kiir kumtuhumu aliyekuwa naibu wake Riek Machar, kwa nia ya kupanga njama ya kupindua serikali yake, hali iliyozua mzozo wa kisiasa, katika taifa hilo changa zaidi duniani.
Mapigano hayo sasa yamechukua mkondo wa kikabila na hivi majuzi juhudi za jamii ya kimataifa kuzipatanisha pande hizo mbili zilifua dafu pale wawili hao walipotia saini mkataba wa amani.

No comments:

Post a Comment