Rais wa Nigeria Muhammadu Buhari anafanya mazungumzo mjini Washington na rais wa Marekani Barack Obama.
Mazungumzo baina ya viongozi hao wawili yanalenga ushirikiano katika vita dhidi ya wanamgambo wa kiislamu wa Boko Haram.
Awali Marekani ilikubali kuisaidia Nigeria katika vita dhidi ya makundi ya uasi hasa baada ya kutekwa nyara kwa wasichana zaidi ya 200 wa shule kutoka Chibok mwaka jana.
Hata hivyo uhusiano baina ya Marekani na utawala ulioondoka madarakani wa Goodluck Jonathan ulidhoofika , baada ya shutuma za makundi ya kutetea haki za kibinadamu kuhusu ukiukaji wa haki za kibinadamu unaotekelezwa na jeshi la Nigeria.
Bwana Buhari pia ameahidi kushughulikia ufisadi na amesema atarejesha mabilioni ya dola yaliyofichwa kwenye benki za Marekani Uswiss na kwingineko.
No comments:
Post a Comment