Komredi Kinana akimtumbukiza mbuzi kwenye josho, katika Kijiji cha Nyakwasi, wilayani Nyan'hwale, Geita.Mbunge wa Jimbo la Nyang'hwale, Hussein Kasu ameshiriki ujenzi wa josho hilo pamoja na malambo 91 jimboni humo. (Picha zote na Richard Mwaikenda, Kamanda wa Matukio Blog)
Komredi Kinana akiswaga ng'ombe ili waingie kwenye josho kwa ajili kuua wadufu katika Kijiji cha Nyakwasi wilayani humo.
Komredi Kinana akilakiwa katika Kijiji cha Bukwimba, ambapo alishiriki kupaka rangi jengo la CCM Kata ya Bukwimba.
Komredi Kinana akishiriki kupaka rangi jengo la Ofisi ya CCM Kata ya Bukwimba wilayani Nyang'wale. mkoani Geita.
Komredi Kinana akishiriki kufukia mabomba ya maji katika Kata ya Bukwimba, wilayani Nyang'hwale, Geita.
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye akihutubia katika mkutano uliofanyika katika Kijiji cha Busolwa, ambapo Komredi Kinana alikagua ujenzi wa Daraja katika Kitongoji cha Mwiza, wilayani Nyang'hwale.
Komredi Kinana akiwasha mashine za kusaga na kukoboa mradi wa akina mama wa Kijiji cha Nyangongwa, wilayani humo.
No comments:
Post a Comment