Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akikagua ujenzi tangi na chujio la maji la mradi wa maji wa Sengerema mjini uliopo eneo la Nyamazugowa, akiwa katika ziara ya kukagua utekelezaji wa ilani ya CCM na uhai wa Chama mkoani Mwanza.
Katibu
Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akikata utepe kuzindua Kivuko Super
Sumar kinachofanya kazi ya kusafirisha abiria, mizigo, na magari kutoka
Bandari ya Kamanda, Sengerema hadi Mwanza. Kivuko hicho kina uwezo wa
kubeba abiria 300 na magari kati ya 20 a 50 kuuatana na ukubwa.
Katibu
Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akihutubia maelfu ya wananchi
waliojitokeza katika mkutano wa hadhara aliofanya katika viwanja vya
Ofisi ya CCM, wilaya ya Sengerema mjini, akiwa katika ziara ya kukagua
utekelezaji wa ilani ya CCM na Uhai wa Chama mkoani Mwanza leo.
Katibu
Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, akiwa na baadhi ta viongozi wa chama
hicho akishuka kwenye kivuko MV Misungwi, alipowasili wilayani Misungwi
kuanza ziara ya kikazi.
Katibu
Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, akiangalia ngoma ya utamaduni wakati
wa mapokezi eneo la Usagara, alipowasili wilayani Misungwi, Mwanza,
kuanza ziara ya kikazi jana, akitokea Jimo la Sengerema. (Picha zote na Richard Mwaikenda)

No comments:
Post a Comment