TANGAZO


Sunday, June 28, 2015

Ziara ya Kinana Jimbo la Nyamagana Mwanza

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Abdulrahman Kinana akihutubia mkutano baada ya kufungua Jengo la Kitega Uchumi la CCM katika Kijiji cha Buhongwa, Jimbo la Nyamagana, jijini Mwanza leo, wakati wa ziara ya kuimarisha uhai wa chama, kukagua utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi pamoja na kusikiliza  kero za Wananchi na kuzitafutia ufumbuzi.
Sehemu ya umati wa watu uliohudhuria katika mkutano ambapo Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana alihutubia na kufungua Jengo la Kitega Uchumi la CCM katika Kijiji cha Buhongwa, Jimbo la Nyamagana, jijini Mwanza.
Wanachama wa Vicoba, Bodaboda, Machinga na Mama Lishe wakimsikiliza kwa makini Komredi Kinana alipokuwa akizungumza nao kuhusu changamoto zinazowakabili, ambapo aliwaahidi kuwafanyia mipango ya kupata mikopo yenye riba nafuu katika Benki ya CRDB na Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya Jamii (NSSF).

No comments:

Post a Comment