TANGAZO


Monday, June 1, 2015

Wizara ya Elimu yashauriwa kutatua changamoto za walimu nchini

Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Dkt. Shukuru Kawambwa akiwasilisha makadirio ya mapato na matumizi ya wizara yake kwa mwaka wa fedha 2015/2016 bungeni mjini Dodoma leo. 
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma za Jamii Bi. Margaret Sitta akiwasilisha taarifa ya kamati hiyo kuhusu utekelezaji wa majukumu ya Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi kwa mwaka wa fedha 2014/2015 leo bungeni mjini Dodoma. 
Mhadhiri Msaidizi Idara ya Mimea kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Bw. Heriel Moshi (kulia) akitoa ufafanuzi kuhusu mbegu za mimea zinazotumika kutengeneza mafuta ya kuendeshea mashine kwenye maonyesho ya chuo hicho yaliyofanyika viwanja vya bunge mjini Dodoma leo. 
 Mtafiti wa masuala ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (ICT) kutoka Chuo Kikuu cha Dar es  Salaam (UDSM), Dkt. Honest Kimaro akionyesha mfumo wa kielektroniki wa ukusanyaji wa taarifa za magonjwa ya mlipuko na utoaji wa huduma za afya nchini kwenye maonyesho ya chuo hicho yaliyofanyika katika viwanja vya Bunge mjini Dodoma leo.
Baadhi ya watu mbalimbali wakipata elimu kuhusu shughuli za utafiti walipohudhuria maonyesho ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam yaliyofanyika kwenye viwanja vya Bunge mjini Dodoma leo. 
Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT) Bw. Ezekia Oluoch (kushoto) akieleza jambo kwa Naibu Waziri wa Fedha Mhe. Mwigulu Nchemba (katikati) pamoja na wabunge Bi. Asumta Mshama na Bw. James Mbatia (kulia) nje ya ukumbi wa Bunge mjini Dodoma leo.
Mbunge wa Viti Maalum Bi. Al-Shaymaa Kwegyir (mwenye nguo nyeupe) akiwa pamoja na wanakwaya wa Moyo Mtakatifu wa Yesu kutoka Singida kwenye viwanja vya Bunge mjini Dodoma leo. (Picha zote na Fatma Salum - Maelezo)

No comments:

Post a Comment