Mh. Waziri wa Fedha Saada Mkuya Salum (MB) akitoa maelekezo kwa Meneja wa TRA mkoani Dodoma (mwenye miwani) na wakala wa TRA kutoka Yono Action Mart kulifunga duka la Salome Furniture baada ya kukutwa akifanya biashara bila ya kutumia risiti za mashine ya EFD.
Mh. Waziri wa Fedha Saada M.Salum(MB) akimsikiliza msimamizi wa duka la Salome Furniture wakati akijitetea baada ya kukutwa anafanya biashara bila ya kutumia mashine ya EFD.
Mh. Waziri wa Fedha Mh. Saada M. Salum (MB) akiwa katika mgahawa wa Dodoma Carnival alipotembelea kukagua matumizi ya mashine za EFD. Mh. Waziri aliagiza mgahawa huo ufungwe mpaka hapo watakaponunua mashine hizo. Kushoto kwa Mh. Waziri ni meneja wa TRA Mkoa wa Dodoma na mwenye shati jekundu ni msimamizi wa mgahawa huo.
Waziri
wa Fedha Mh. Saada Mkuya Salum (MB) akiwa na Mh. Rukia Kassim Ahmed Mbunge wa
viti maalum kupitia Chama cha Wananchi CUF wakitoka kwenye duka ambalo
lilikutwa mmiliki wake akifanya biashara bila ya kutoa risiti za mashine ya
EFD.
Na Msemaji Mkuu,
Wizara ya Fedha, Dodoma
Mh. Waziri wa Fedha Saada Mkuya Salum amefanya ukaguzi
wa ghafla katika baadhi ya maduka Mkoani Dodoma ili kuona kama maelekezo ya
Serikali kuhusu matumizi ya mashine za EFD yanatekelezwa ipasavyo.
Katika ukaguzi huo ambao ulihusisha maduka ya kuuza
thamani za majumbani, nguo na maduka ya kuuza bidhaa mchanganyiko (Min
supermarket), Mh. Waziri akiongozana na Watumishi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania
aliagiza kufungwa kwa maduka yote ambayo yamekaidi agizo la Serikali la
matumizi ya mashine EFD mpaka pale watakaponunua na kuzitumia ipasavyo mashine
hizo.
Aidha Mh. Waziri amewataka wafanyabiashara na wananchi
kwa ujumla kuisaidia Serikali kuwafichua wafanyabiashara wasio waaminifu na
ambao wanapelekea kuikosesha Serikali mapato ambayo yangetumika katika
kuboresha huduma za kijamii.
No comments:
Post a Comment