TANGAZO


Friday, June 19, 2015

Watu 35 wafa kwa kunywa gongo India

Mtu aliyekunywa pombe haram akihudumiwa
Watu wapatao 35 wamekufa katika mji wa Mumbai nchini India baada ya kunywa pombe haramu.
Wengi wao wamelazwa hospitali.
Waziri kiongozi wa jimbo la Maharashtra ametaka ufanyike uchunguzi, watu watatu wamekamatwa.
Pombe haramu aina ya gongo inayotokana na mahindi inanyweka kwa kiasi kikubwa nchini kote India ambako wakati mwingine pombe hiyo inauzwa chini ya dola moja ya Kimarekani, ikisababisha vifo vya mara kwa mara.
Karibu watu 170 wameripotiwa kufa katika jimbo la Bengal baada ya kunywa pombe hiyo maarufu kama "moonshine"

No comments:

Post a Comment