TANGAZO


Tuesday, June 30, 2015

Watia nia wa CCM warudisha fomu za kuomba kuteuliwa kugombea Urais

Mfanyakazi wa Chama Cha Mapinduzi Makao Makuu, Dodoma, Mambo ya Nje, Amos Siyantemi akishangilia na wafuasi wake, alipokuwa akirejesha fomu za kuomba kuteuliwa na chama chake katika nafasi ya Urais wa Muungano kwa Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara, Rajabu Luhavi, ofisini hapo leo. (Picha zote na John Banda)
Mfanyakazi wa Chama Cha Mapinduzi Makao Makuu, Dodoma, Mambo ya Nje, Amos Siyantemi akirejesha fomu za kuomba kuteuliwa na chama chake katika nafasi ya Urais wa Muungano kwa Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara, Rajabu Luhavi, ofisini hapo leo.
Dk. Joseph Shaggama, akirejesha fomu za kuomba kuteuliwa kwa nafasi hiyo kwa Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara, Rajabu Luhavi, ofisini hapo leo.
Dk. Joseph Shaggama, akizungumza na waandishi wa habari baada ya kurejesha fomu za kuomba kuteuliwa kwa nafasi hiyo kwa Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara, Rajabu Luhavi, ofisini hapo leo.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe (kulia), akirejesha fumu hizo.
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe (kulia), akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kurejesha fumu hizo.
Kada wa CCM, Monica Mbegga (kulia), akikabidhi fomu zake za kuomba kuteuliwa kwa Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara, Rajabu Luhavi, ofisini hapo leo.
Kada wa CCM, Monica Mbegga (kulia), akizungumza na waandishi wa habari, mara baada ya kukabidhi fomu zake za kuomba kuteuliwa kwa Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara, Rajabu Luhavi, ofisini hapo leo.
Waziri Afrika Mashariki Dk. Harson Mwakyembe (kulia), akirejesha fomu zake za kuomba kuteuliwa na Chama chake cha Mapinduzi (CCM) kwa nafasi ya kuwania Urais kupitia chama hicho, kwa Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara, Rajabu Luhavi, ofisini hapo leo.
Kada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. Mwele Malecela, akikabidhi fomu zake za kuomba kuteuliwa na chama chake hicho kwa nafasi ya Urais mjini Dodoma leo.
Kada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. Mwele Malecela, akikabidhi fomu zake za kuomba kuteuliwa na chama chake hicho kwa nafasi ya Urais mjini Dodoma leo.
Kada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Dk. Mwele Malecela, akiwapungia mashabiki wake, wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari, mara baada ya kukabidhi fomu zake za kuomba kuteuliwa na chama chake hicho kwa nafasi ya Urais mjini Dodoma leo.
Waziri Mkuu Mizengo Pinda, akizunguma na waandishi wa habari, mara baada ya kukabidhi fomu zake za kuwania nafasi hiyo, kwa Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara, Rajabu Luhavi, Makao Makuu ya CCM, mjini Dodoma leo.
Waziri Mkuu wa mstaafu, Fredrick Sumaye, akikabidhi fomu za kuomba kuteuliwa kwa nafasi ya Urais kupitia CCM kwa Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara, Rajabu Luhavi mjini Dodoma leo.
Waziri Mkuu wa mstaafu, Fredrick Sumaye, akizungumza na waandishi wa habari, mara baada ya kukabidhi fomu za kuomba kuteuliwa kwa nafasi ya Urais kupitia CCM kwa Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara, Rajabu Luhavi mjini Dodoma leo. 

No comments:

Post a Comment