TANGAZO


Sunday, June 21, 2015

Upinzani washtumu kuondoka kwa Bashir

Rais Omar el Bashir awasili nchini Sudan baada ya kutoka nchini Afrika ya kusini
Chama cha upinzani nchini Afrika ya Kusini kimetaka uchunguzi kufanywa nchini humo kufuatia hatua ya serikali kushindwa kumkamata rais wa Sudan Omar el Bashir ambaye ameshtakiwa na mashtaka ya mauaji ya kimbari katika mahakama ya ICC.
Bwana Bashir alikuwa nchini Afrika kusini wiki iliopita kwa mkutano wa viongozi wa Afrika lakini alikaidi agizo la mahakama la kumtaka asalie nchini humo.
Chama cha muungano wa Kidemokrasia kimesema kuwa kinataka kujua ni nani aliyemruhusu bwana Bashir kuondoka nchini humo.
Kinasema kuwa serikali ilihusika katika mpango wa kumsaidia kuondoka nchini humo.

No comments:

Post a Comment