TANGAZO


Saturday, June 27, 2015

Ulaya yakataa kuiongeza Ugiriki muda zaidi

Uchumi mbaya wazua wasiwasi Ugiriki
Mawaziri wa fedha wa mataifa ya ulaya wamekatalia mbali ombi la Ugiriki la kutaka iongezewa muda zaidi wa kulipa deni lake kutoka Jumanne ijayo.
Ugiriki ina hadi Jumanne ijayo kulipa deni lake la zaidi ya dola bilioni moja nukta saba.
Serikali ya Uigiriki chini ya Alexis Tsipras ilikuwa imeombamuda wa majuma mawili iliiandae kura ya maoni
kuhusu makubaliano yaliyopendekezwa na wakopeshaji wa kimataifa wa nchi hiyo.
null
Waziri mkuu nchini Ugiriki Alexis Tsipras,anatarajiwa kuomba muda zaidi wa kulipa deni la IMF
Ikiwa itaidhinishwa kura hiyo itafanyika tarehe tano mwezi Julai.
Awali wagiriki walipiga foleni nje ya mabenki wakihofia kuwa watawekewa masharti dhidi ya kutoa pesa zao.
Mwandishi wa BBC mjini Athens anasema kuwa kulikuwa na uvumi kuwa kiwango kipya cha pesa ambacho mtu anaweza kutoa kwa benki kinaweza kuwa euro 80.
Bunge la Ugiriki nalo liliandaa kikao cha dharura kujadili pendekezo ya kufanyika kwa kura hiyo ya maoni.
Waziri mkuu nchini Ugiriki Alexis Tsipras, anasema kuwa masharti hayo yanayotaka kupunguzwa kwa matumizi ya umma hayawezi kustahimiliwa.
null
Watu nchini Ugiriki wameanza kupanga foleni nje ya mabenki wakihofia kuwa watawekewa masharti dhidi ya kutoa pesa zao.
Baadaye atakutana na waziri wa fedha wa nchi za ulaya mjini Brussels kuomba kuongezwa muda zaidi wa kulipa kwa mkopo wa sasa wa Ugiriki.
Muda unazidi kuyoyoma kwa bwana Tsipras kuwa amelipa deni la dola mbilioni 1.7 kwa shirika la IMF ifikapo jumanne ijayo..

No comments:

Post a Comment