Waziri wa fedha wa Ujerumani Wolfgang Schaeuble ameonya kuwa tofauti iliopo kati ya Ugiriki na wakopeshaji wake wa kimataifa inazidi kuongezeka.
Mawaziri wa fedha wa mataifa ya bara Ulaya wanaokutana mjini Brussels kwa mara ya nne katika kipindi cha wiki moja, wanasema kuwa Ugiriki imerudi nyuma zaidi.
Katika mkutano wa awali na Waziri mkuu wa Ugiriki Alexis Tsipras, wakopeshaji walipendekeza kupunguzwa kwa malipo ya uzeeni na kuondoa ushuru mdogo kwa raia walioko katika visiwa vya Ugiriki.
Waziri Tsipras amekataa kata kata kupunguza malipo ya uzeeni akisema itahujumu uwezo wa Wagiriki ambao hawana kitega uchumi kuendelea kujikimu kimaisha.
Awali Mawaziri wa mashauri ya nchi za kigeni wa Bara Ulaya walikutana kutafuta mbinu ya kuisaidia Ugiriki.
Shirika la fedha Duniani- IMF, linataka serikali ya Ugiriki ambayo ilipendekeza kukata matumizi ya fedha na kuongeza ushuru Jumatatu na kupunguza matumizi zaidi kabla ya kuokolewa.
Athens, inahitaji msaada wa kifedha kulipa madeni yake kufikia mwisho wa mwezi huu.

No comments:
Post a Comment