Uingereza imeonya kuwa wapiganaji Waislamu wanaweza kufanya mashambulio mengine dhidi ya watalii nchini Tunisia.
Wizara ya mashauri ya nchi za nje ya Uingereza, ilisema mashambulio hayo yanaweza kufanywa na watu ambao wakuu hawa-wa-jui, na ambao wame-vu-tiwa na magaidi katika mitandao ya kijamii.
Kati ya watalii 38 walio-uliwa pwani ya mji wa Sousse, 15 walikuwa Wangereza.
Jana usiku maelfu ya watu wa mji huo waliandamana kulaani shambulio hilo.
Na mamia ya polisi wenye silaha wamewekwa sehemu za pwani, zinazopendwa na watalii.
Maelfu ya watalii wameondoka nchini Tunisia kufuatia shambulizi hilo la siku ya Ijumaa kwenye eneo moja la ufuo wa bahari ambapo watu 38 waliuawa wengi wakiwa kutoka ulaya.
Afisa anayehusika na masuala ya utalii katika eneo la Sousse amesema kuwa wageni zaidi ya 3000 wameondoka eneo hilo tangu mauaji hayo yafanyike.
Serikali mjini Tunis inasema kuwa usalama umedumishwa lakini makampuni ya watalii tayari yameanza kufuta safari.
Kundi la Islamic State linasema kuwa ndilo lililohusika kwenye shambulizi hilo.
No comments:
Post a Comment