Kaimu Mkurugenzi
Maendeleo ya Vijana kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bibi.
Venerosa Mtenga (kulia) akizungumza na ujumbe kutoka Nchi ya Zimbabwe waliofika
katika ofisi za Wizara hiyo jana jijini Dar es Salaam kujifunza namna Wizara inavyosimamia uendeshaji wa Mfuko wa Maendeleo ya
Vijana. Kushoro ni Kaimu Mkurugenzi wa uwezeshaji uchumi kutoka Wizara ya
Vijana, na uwezeshaji Uchumi nchini Zimbabwe Bw. Tafi Greemas Mashonganyika.
Kaimu Mkurugenzi wa uwezeshaji
uchumi kutoka Wizara ya Vijana, na uwezeshaji Uchumi nchini Zimbabwe Bw. Tafi
Greemas Mashonganyika (aliyesimama) akielezea lengo la ujio wake na wajumbe
kadhaa nchini Tanzania baada ya kukutana na maafisa vijana wa Wizara ya Habari,
Vijana, Utamaduni na Michezo jana jijini Dar es Salaam. Katikati ni Kaimu Mkurugenzi
Maendeleo ya Vijana Bibi. Venerosa Mtenga na Kulia ni Kaimu Katibu Mkuu Wizara
ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bw. Barnabas Ndunguru.
Ofisa Maendeleo ya Vijana
kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bw. Eliakim Mtawa akitoa
mada ya uendeshaji na usimamizi wa Mfuko wa Maendeleo ya Vijana kwa ujumbe
kutoka nchini Zimbabwe waliofika Tanzania kujifunza juu ya Mfuko huo jana
Jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Fedha
na Utawala kutoka Wizara ya Vijana, na uwezeshaji Uchumi nchini Zimbabwe Bw.
Emmanuel Ngwarati (mwenye miwani) akichangia mada wakati wa mkutano kati ya
maafisa Vijana kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo na ujumbe
kutoka Nchi ya Zimbabwe waliofika Wizarani hapo jana jijini Dar es Salaam kujifunza
namna Wizara inavyosimamia uendeshaji wa Mfuko wa Maendeleo ya Vijana. Kulia ni
Kaimu Mkurugenzi wa uwezeshaji uchumi kutoka Wizara ya Vijana, na uwezeshaji Uchumi
nchini Zimbabwe Bw. Tafi Greemas Mashonganyika.
Maofisa Vijana kutoka
Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo pamoja na ujumbe kutoka Wizara
ya Vijana na uwezeshaji Uchumi nchini Zimbabwe wakifuatilia kwa makini mada
mbalimbali zilizokua zikiendelea wakati wa ziara ya kujifunza juu ya uendeshaji
na usimamizi wa Mfuko wa Maendeleo ya Vijana nchini Tanzania.
Ofisa Sera na Mipango
kutoka Wizara ya Vijana na uwezeshaji Uchumi nchini Zimbabwe Bi. Klery Chikwede
(aliyepiga magoti) akimkabidhi Kaimu Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana,
Utamaduni na Michezo Bw. Barnabas Ndunguru (kulia) zawadi kama shukrani kwa
Wizara kukubali kuwapokea na kuwapa elimu ya uendeshaji na usimamizi wa Mfuko
wa Maendeleo ya Vijana. Katikati ni Kaimu Mkurugenzi Maendeleo ya Michezo Bibi.
Venerosa Mtenga.
Kaimu Mkurugenzi
Maendeleo ya Vijana Bibi. Venerosa Mtenga katika picha ya pamoja ya Maofisa
Vijana kutoka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo pamoja na ujumbe
kutoka Wizara ya Vijana na uwezeshaji Uchumi nchini Zimbabwe wakati wa ziara ya
ujumbe huo nchini Tanzania kujifunza juu ya uendeshaji na usimamizi wa Mfuko wa
Maendeleo ya Vijana.
No comments:
Post a Comment