Mkurugenzi wa Vision Investments, Ally Nchahaga, akizungumza na waandishi wa habari, Dar es Salaam leo, kuhusu mnada wa magari (automart), utakao wakutanisha wauzaji na wanunuzi wa magari, viwanja vya Hoteli ya Sea Cliff, Juni 28, mwaka huu jijini. Kushoto ni Ofisa Masoko, Rehema Magogo na kulia ni Ofisa Uhusiano, Fatma Hamisi. (Picha na Kassim Mbarouk)
KWA mara ya kwanza Tanzania, Automart inawaletea mbadala sahihi wa kutimiza mahitaji yako yote ya magari. Kila Jumapili ya mwisho wa mwezi wauzaji na wanunuzi wa magari watakutana katika mazingira rafiki.
Makutano haya baina ya wateja kwa wateja na wanunuzi na wateja;yatafanyika katika viwanja vya Sea Cliff Hotel, Dar es Salaam. Automart itafunguliwa tarehe 28 Juni 2015 kuanzia saa 3 asubuhi hadi saa 11 Jioni.
Makutano haya yameandaliwa kuwapa fursa wanunuzi na wauzaji wa magari binafsi na makampuni tofauti fursa ya kuwa na sehemu moja kwa mahitaji yote.
Pamoja na hayo tunaalika huduma shirikishi zikijumlisha kampuni za bima, taasisi za fedha wanao toa mikopo ya magari, Vilainishi vya magari na Kliniki za magari kutoa huduma.
Kwa mtu yeyote anae hitaji kuuza gari lake atachangia Shilingi elfu 50 tu. Ikiwa ni mchango wakuweka gari lake katika viwanja vya Automart na kufaidika na kuwekwa katika mtandao wa jamii (facebook) unao fanyiwa promotion kwa mwezi.
Automart inatoa nafasi za udhamini na maonesho. Kampuni ya Vision Investment inakaribisha wadhamini na watu wanaotaka kushiriki.
Kuhusu Vision Investments
Vision Investments ni moja ya sehemu ambapo mawazo ya mikakati mbalimbali na teknolojia mpya inapohitajika ili kuweka biashara katika mstari wa mbele. Malengo ya Vision ni kutambua, kuunda, kuendeleza, kutoa na kuuza masuluhisho yanayofaa kukidhi mahitaji ya mteja ili kuhakikisha ufanisi wa hali ya juu, uwezo na thamani.
Vision pia ni wataalamu wa mtandao, ushauri wa Masoko na usimamizi wa matukio.
Kwa taarifa zaidi, tembelea: HYPERLINK "http://www.vision.co.tz" www.vision.co.tz
No comments:
Post a Comment