TANGAZO


Friday, June 5, 2015

SKYLIGHT BAND yaendelea kuunguruma ndani ya Kiota kipya cha Lukas Pub Masaki jijini Dar leo

Ilikuwa noma sana siku ya Ijumaa iliyopita maana ilikuwa sio ya kupitwa basi mchuke na ndugu, jamaa au rafiki yako leo uje kuona vitu vitamu kutoka kwenye Bendi ya Skylight.
Meneja wa Skylight Band Aneth Kushaba AK 47 akiimba moja ya nyimbo yenye hisia kali sambamba na msanii mwenzake Sam Mapenzi.
Mwimbaji kutoka Bendi ya Skylight, Sony Masamba akitoa burudani ndani ya kiota cha Lukas Pub huku akisindikizwa na wasanii wenzake ambao ni Meneja wa Skylight Band Aneth Kushaba AK 47(katikati) na Sam Mapenzi.
Sam Mapenzi pamoja (Kushoto) na Ashura Kitenge wakiimba kwafuraha huku wakiwakonga nyoyo mashabiki wa Skylight Band.
Rapa mkongwe kwenye muziki wa Live Joniko Flower akishusha mistari na kucheza huku waimbaji wenzake Sony Masamba (wa pili kutoka kushoto), Aneth Kushaba(wa pili kutoka kulia) pamoja na Sam Mapenzi wakisebeneka Ijumaa iliyopita ndani ya kiota cha Lukas Pub jijini Dar.
Sony Masamba akiimba na kucheza pamoja na waimbaji wenzake ambao ni Aneth Kushaba (katikati) pamoja na Sam Mapenzi ndani ya kiota kipya cha Lukas kilichoko Masaki jijini Dar.
Rapa mkongwe kwenye muziki wa Live Joniko Flower akiimba na kusheza pamoja na waimbaji wenzake kwenye kiota cha Lukas Pub ijumaa iliyopita
Ulikuwa ni mwendo wa kuserebuka mbele ya mashabiki wao(hawapo pichani) maana ilikuwa ni noma saanaaaaa.....!!!!
Binti mwenye sauti ya kumtoa Nyoka pangoni, Ashura Kitenge akiimba kwa hisia moja ya nyimbo inayobamba sana nje na ndani ya Tanzania katika kiota cha Lukas Pub jijini Dar.
Meneja wa Skylight Band, Aneth Kushaba AK47 akiimba sambamba na msanii mwenzake Ashura Kitenge.
Waimbaji wa Skylight Band wakiendelea kutoa burudani ya kukata na shoka.
Meneja wa Skylight Band, Aneth Kushaba AK47 akiendelea kutoa burudani huku akisindikizwa na wasanii wenzake ambao ni Ashura Kitenge(wa kwanza kutoka kushoto), Joniko Flower(wa pili kutoka kushoto) pamoja na Sony Masamba.
Ulifika wakati wa kuanza kucheza style za bendi ya Skylight hii ni style ya Kikuku inakubidi kanza usugue alafu ufanye ya kwako njoo leo ujionee mambo mapya kutoka katika bendi yako.
Mashabiki wa Skylight Band wakijiachia kwa raha zao ndani ya kiota cha Lukas pub.
Sam Mapenzi akitoa burudani huku akisindikizwa na wanamziki wenzake waliokuwa wakimpa support ya nguvu kwenye ngoma za Nigeria ambao ni Joniko Flower (wa kwanza kushoto), Ashura Kitenge(wa pili kutoka kulia) pamoja na Sony Masamba.
Ilikuwa ni furaha maana Fleva zilizokuwa zikipigwa zilikuwa zinawapagawisha mashabiki.
Meneja wa Skylight Band, Aneth Kushaba AK47 akiimba.

No comments:

Post a Comment