TANGAZO


Wednesday, June 17, 2015

Serikali ya muungano Palestina imevunjika

Abbas
Serikali ya Palestina iliobuniwa ili kuponya mgawanyiko kati ya makundi ya Hamas na Fatah imevunjika.
Waziri wake mkuu Rami Hamdallah amejiuzulu rasmi.
Hatua hiyo inajiri baada ya rais Mahmoud Abbas kuliambia kundi lake la Fatah kwamba serikali hiyo ya mwaka mmoja itavunjika kwa kuwa Hamas imekataa kuiruhusu kufanya oparesheni zake katika huko Gaza.
Hatahivyo Hamas limesema kuwa halikushauriwa na kwamba linapinga mpango wowote wa kuvunjwa kwa utawala huo.

No comments:

Post a Comment