Mkurugenzi wa Muungano, Ofisi ya Makamu wa Rais Bw. Baraka Rajab Baraka akitoa wito kwa wananchi kulinda, kuudumisha na kuendeleza muungano ili kuwa na nchi yenye umoja, amani na usalama, wakati wa mkutano uliofanyika katika ukumbi wa Idara ya Habari (MAELEZO) leo Jijini Dar es Salaam.Kushoto ni Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Makamu wa Rais Mhandisi Angelina Madete.
Kaimu Mkurugenzi Uzingatiaji na
Ufuatiliaji wa Sheria kutoka Baraza la Taifa la Mazingira (NEMC) Ruth Lugwisha
akiwaasa wananchi kubadili tabia na kuacha kutumia mifuko ya plastiki
isiyoruhusiwa ili kuepuka uchafuzi wa Mazingira na Athari zake, wakati wa
mkutano uliofanyika katika ukumbi wa Idara ya Habari (MAELEZO) leo Jijini Dar
es Salaam. Kulia ni Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Mazingira, Ofisi ya Makamu wa
Rais Bw. Richard Muyungi. (Picha zote na Hassan Silayo-MAELEZO)
Na Frank Mvungi-MAELEZO
SERIKALI imeendelea kuimarisha umoja,amani na utulivu miongoni mwa wananchi wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania katika kipindi cha miaka kumi.
Hayo yamesemwa na Naibu Katibu Mkuu
Ofisi ya Makamu wa Rais Mhandisi Angelina Madete wakati wa mkutano na vyombo vya habari leo jijini Dar es salaam.
Mhandishi Madete alisema kuwa suala la
muungano ni miongoni mwa vipaumbele vya Serikali ya awamu ya nne kwa dhumuni la kuimarisha umoja na utulivu
nchini.
“Serikali ya awamu ya nne inajivunia
uimarikaji wa Umoja, amani na utulivu miongoni mwa wananchi ya Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania kwani ilikuwa ni moja ya kipaumbele kilichowekwa na
serikali hii katika kipindi cha miaka Kumi ya Uongozi wa Rais Dkt. Jakaya
Kikwete.” Alisema Mhandisi Madete.
Mhandishi Madete aliongeza kuwa Taasisi
za Muungano kama Ulinzi na Usalama,Uhamiaji na Uraia,Fedha , Sarafu na
Mawasiliano zimeendelea kuimarika kwa kutoa huduma bora kwa wananchi katika
kipindi cha Serikali ya awamu ya nne.
Akifafanua Madete amesema katika
kipindi cha awamu ya nne wananchi wa pande zote mbili za muungano wameendelea
kunufaika na shughuli za kiuchumi na kuongeza ajira kupitia utekelezaji wa
program za maendeleo ikiwemo mfuko wa maendeleo ya jamii (TASAF),Progamu ya usimamizi wa Bahari na
Pwani (MACEMP) na mradi wa kutoa mikopo kwa ajili ya miradi midogomidogo
(SELF).
Miradi mingine ni program ya
maendeleo ya Sekta ya Kilimo (ASDP) , mradi shirikishi wa program za maendeleo
ya kilimo( PADEP) na program yamaendeleo ya Mileninia ambayo kwa pamoja
imewanufaisha wananchi kwa kuwaletea maendeleo endelevu.
Mafanikio mengine ni ujenzi wa
majengo ya Taasisi za Muungano ikiwemo kukamilika kwa ujenzi wa Ofisi ya Makamu
wa Rais,Mtaa wa Lithuli,Dar es salaam,awamu ya pili ya ujenzi wa ofisi ya
Makamu wa Rais Tunguu-Zanzibar umekamilika kwa kiwango kikubwa.
Pia ujenzi wa Tawi la Benki Kuu
lililopo Gulioni Zanzaibar umekamilika ambapo majengo mengine yaliyojengwa ni
pamoja na uhamiaji,Makao makuu na Ofisi za BungeTunguu na Tume ya Sayansi na
Teknolojia (COSTECH).
No comments:
Post a Comment